Skip to main content

RIPOTI YA MCHANGO WA ELIMU YA URAIA SHULE ZA SEKONDARI YAZINDULIWA NA HAKI ELIMU.

 

  RIPOTI YA UTAFITI KUANGALIA MCHANGO WA ELIMU YA URAIA SHULE ZA SEKONDARI YAZINDULIWA NA HAKI ELIMU.  

 Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari akizindua ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchin, hafla hiyo imefanyika  Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari wakionesha ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchin, hafla hiyo imefanyika  Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam.Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika  Jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mkuu HakiElimu Bw.Godfrey Bonventure akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika  Jijini Dar es Salaam.

 Dar es Salaam

Katika kuendeleza suala la elimu ya uraia hapa nchini ni,Asasi isiyo ya kiserikali ya HakiElimu  imezindua matokeo ya utafiti katika ngazi ya elimu ya uraia Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Demokrasia nchini  ambapo umeonesha elimu ya uraia inayotolewa  shuleni ina mchango  kidogo katika kumsaidia kijana wa kitanzania kujifunza na kushiriki shughuli za kisiasa na demokrasia. 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akizindua ripoti ya utafiti huo, Kamishna wa Elimu hapa nchini   Dk Lyabwene  Mtahabwa amesema kuwa utafiti huo umekuja wakati muafaka ambapo Rais Samia ametoa maagizo yafanywe mapitio ya mitaala ya elimu ya Tanzania Ili kuwajengea uwezo wanafunzi waweze kuona fursa katika mazingira yao na waweze kujitegemea.



Amesma kuwa, katika kujenga demokrasia ya kweli ni elimu ya uraia lazima ipewe uzito wa hali ya juu kwa kumpa mtoto thamani yake ya utoto na kumuacha afurahie utoto wake , huku akiitaka jamii kuonesha uzalendo wa kweli ule ambao unatoka moyoni Ili kwa pamoja tuweze kuimarisha ulizi na usalama wa mtoto popote atakapokuepo afurahie utoto wake.


Hata hivyo ameongeza kuwa wao kama serikali wametapokea mapendekezo yaliyopo katika utafiti huo ambao ameutaja kama mazuri mno na ambao umekuja  kwa wakati muafaka na itachukua mapendekezo hayo na kuyapeleka   katika kamati ya kitaifa iliyoundwa kupitia mitaala ya masomo.


Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi HakiElimu Godfrey Bonveture amesema kuwa,utafiti uliofanyika na Asasi ya HakiElimu umebaini kuwepo kwa changamoto kubwa katika mtaala wa somo la uraia Shule za Sekondari ambao kwa kiwango kikubwa haumpi  mafunzo stahiki Mwanafunzi yatakayomfanya aelewe vyema namna ya kushiriki shughuli za kidemokrasia.


Aidha, amesema, kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa kwa wilaya 10 umeonesha ushiriki hafifu kwa vijana katika mifumo ya kidemokrasia ndani na nje ya shule ambapo asilimia 44.4 wanafunzi hawaelewi maana ya demokrasia huku asilimia 85.5 hawajawahi kushiriki wala kushirikishwa katika vikao rasmi vya maamuzi kuhusu mapato na mgawanyo wa rasilimali za shule .


"utafiti huu pia umeonesha asilimia 47 ya viongozi wa wanafunzi shule za Sekondari hawapatikani kwa njia ya chaguzi za demokrasia bali kwa kuteuliwa na uongozi wa shule,huku katika ngazi ya jamii zaidi ya asilimia 80 ya vijana walioko shuleni hawajawahi na hawahamasishwi kushiriki mikutano ya kampeni na siasa"amesema Bonveture. 


Aidha, wazazi na walezi wametakiwa kuachana na mfumo wa malezi usiowashirikisha watoto au unaowatenga katika maamuzi ya kifamilia na maslahi yao, pamoja na kuwashirikisha watoto katika kuchagua katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, fani, upangaji wa bajeti za kifamilia na uendeshaji wa mipango ya kifamilia kidemokrasia badala ya kuamuliwa kila kitu.


Katika hatua nyingine, wameiomba Serikali kuboresha ufundishaji wa somo la uraia darasani kwa kusisitiza Mawasiliano ya karibu zaidi kati ya Mwalimu na Mwanafunzi na kuchanganya mbinu za darasani na nyengine kama matumizi ya magazeti vipindi vya radio na Tv na kuwashirikisha watoto katika vikao au shughuli zinazohusisha siasa za demokrasia katika ngazi ya shule.


Uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo umefanyika katika hoteli ya New,Afrika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo wanafunzi wa shule za sekondari.


Comments