Skip to main content

TAMASHA LA "REJOICE" KUTIKISA DAR,WAZIRI NAPE KULINOGESHA.

 

 TAMASHA LA "REJOICE" KUTIKISA DAR,WAZIRI NAPE KULINOGESHA.





Dar es salaam.
Lile tamasha kubwa la kusifu na kuabudu hapa nchini maarufu kama Rejoice linatarajiwa kufanyika septemba 16 mwaka huu huku mgeni rasmi katika tamasha hili akitarajiwa kuwa waziri wa Teknolojia ya Habari na mawasiliano,Nape Mnauye

Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mratibu wa tamasha hilo ambaye pia ni mlezi wa wa kwaya ya Efatha Moravian Yona Sonelo esema kubwa tamasha hilo kubwa la Kusifu na Kuabudu la Rejoice chini ya kwaya moravian efatha choir, ambalo linakutanisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka Afrika septemba 16, 2022 uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

  Kuhusu.maandalizi ya tamasha hilo Bw Sonela amewaambia wanahabari kubwa kwa sasa yamefikia Asilimia 95  Kabla kuelekea siku ya tamasha ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya watanzania.

Aidha ameongeza kwa siku ya kesho (leo) kwaya Moravian itaanza mazoezi ya mitambo ya sauti na siku ya alhamisi kwaya waalikwa ambapo watafanya mazoezi ikiwemo kwaya maarufu ya  joyous celebration kutoka nchini Afrika kusini.

Amesema Siku hiyo ya Tamasha tarehe 16 ya mwezi wa huu mgeni Mgeni Rasmi atakuwa ni waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Mnauye atahudhuria tamasha hilo kama mgeni Rasmi.

Hata hivyo amesisitiza  kuwa tamasha la rejoice litaanza kuanzia saa 11 jioni ambapo ameongeza kuwa waimbaji wataanza kutumbuiza mpaka alfajiri ya Tarehe 17 yaani siku ya jumamosi.

Kuhusu suala la usalama amewaondoa hofu wahudhuriaji wa tamasha hilo kutokuwa na hofu juu ya usalama wao na mali zao akisisitiza kubwa Usalama siku ya tamasha utakuwa wa uhakika kwani jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha watu wote wanakuwa salama muda wote wa tamasha hilo litakalofanyika.

"tiketi Bado zinapatikana Katika app ya 'NILIPE' ambazo zinaanzi VIP shilingi milioni moja, laki tano, laki moja, Elfu hamsini na elfu ishirini kwa kawaida.

"Tunawakaribisha watanzania wote Katika Tamasha la kuombea Nchi yetu ya Tanzania na Kwa wengine wanaotaka kununua tiketi uwanjani pia zitapatikana" alisema Bw Sonela.

Tamasha la Rejoice 2022 litapambwa na kwaya mbalimbali za muziki wa Injili litafanyika September 16 katika uwanja wa Uhuru,manispaa ya Temeke, jijini Dar es salaam.

Comments