UREJESHO TV ,YAZINDULIWA YAWA MFUMO BORA WA MAWASILIANO,KULITANGAZA NENO LA MUNGU BARANI AFRIKA.

 UREJESHO TV ,YAZINDULIWA YAWA MFUMO BORA WA MAWASILIANO,KULITANGAZA NENO LA MUNGU BARANI AFRIKA.




 Na Judith Chao,Dar es salaam

KATIKA kuunga mkono jitihada za serikali chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Kanisa la RGC Miracle Centre linatarajia kufanya tamasha la muziki wa Injili mwezi,Disemba mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo lenye lengo la kulimbea Taifa amani na upendo pamoja na kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Dar es Salaam  Mkurugenzi wa kanisa hilo, Nabii Peter Nyanga alipokuwa akizindua Tv ya kanisa hilo iitwayo ‘Urejesho’ amesema wana mpango wa kufanya tamasha kubwa ambalo litawakutanisha watu wengi ikiwemo wahubiri mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

“Tumeanza na jambo la kuzindua televisheni yetu ambayo itakuwa inaonyesha mambo mbalimbali katika nchi 34 za Afrika, ila Disemba tuna mpango wa kufanya tamasha kubwa la nchi."

Aidha, Nyanga amesema wanahitaji tamasha hilo liwe kubwa ili kuliombea Taifa pamoja na Rais Samia kutokana na mambo makubwa anayoyafanya.

“Nimefungua televisheni hii kutokana na kipindi cha uviko 19 mwaka 2020 nilipata tabu katika suala la kutoa mahubiri kwa wananchi hivyo ikatulazimu tutafute njia sahihi ya kufikisha neno la kiroho Kwa njia ya televisheni."

Comments