VIJANA WENGI WANA MAONO MAKUBWA HUWEZI KUYAFAHAMU KIURAHISI BILA KUKAA NA KUZUNGUMZA NAO” KENANI KIHONGOSI

 "VIJANA WENGI WANA MAONO MAKUBWA HUWEZI KUYAFAHAMU KIURAHISI BILA KUKAA NA KUZUNGUMZA NAO” KENANI KIHONGOSI


Na Thadei PrayGod

Dar es salaam.

Katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM),Taifa,(Kenani KIHONGOSI amesema vijana wengi hapa nchini wana maono makubwa lakini ili kuyafahamu kiundani zaidi inabidi kukaa na kuzungumza nao.

Katibu huyo aliyasema hayo jijini Dar es salaam jana wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na vijana wa mkoa huo juu ya mambo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumzia lengo la mkutano huo KIHONGOSI alisema kuwa ni kukutana,kubadilishana mawazo,kusikiliza kero na changamoto za vijana pamoja na kupata maoni yao  ili yafanyiwe kazi na serikali inayoongozwa na chama hicho katika kuhakikisha maslahi ya vijana yanawanufaisha vijana wote wenye nia njema na Taifa.

Aidha aliongeza kuwa chama hicho kitahakikisha agenda zote za vijana zinafanyiwa kazi ikiwemo   mawazo yao na kutatuliwa kwa changamoto zao.

Alisema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaamini vijana kwa kiasi kikubwa katika kuipeleka serikali anayoiongoza katika dira ya mafanikio ya Taifa kwa ujumla na ndiyo maana amewapa nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya serikali ili kwa pamoja Taifa lipate maendeleo na majawabu ya kero na changamoto za watanzania kwa ujumla wakiwemo vijana wenyewe.

“ndugu wanahabari vijana wa Tanzania ni vijana wanaojituma hivyo kama jumuiya ya vijana wa CCM nikaweka utaratibu wa kukutana nao na kusikiliza kero na changamoto zao,na pia kusikiliza ushauri na maoni yao juu ya utendaji kazi wa serikali na wapi tunapopaswa kuparekebisha”alisema ndugu Kenani KIHONGOSI 

Kuhusu chaguzi ambazo zinaendelea ndani ya jumuiya hiyo katibu huyo mkuu wa UVCCM Taifa,alisema kuwa mchakato wake unaendelea vizuri huku akiwataka wasimamizi wa chaguzi hizo kuzisimamia kwa haki na kuhakikisha vijana wote watakaopitishwa kugombea nyadhifa mbalimbali wanakidhi vigezo vya kiuongozi.


Hata hivyo amewataka watendaji ambao wana nia ya kuwabeba wagombea wao wasio na sifa waache tabia hiyo kwani chama hicho hakitokubali jambo hilo litokee huku akiwataka wagombea wote vijana wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya UVCCM kuwa waadilifu,wavumilivu na wenye nidhamu ili watakapochaguliwa wakitumikie vyema chama hicho.


Sep 09 2022

Comments