ACT WAZALENDO YATOA USHAURI MZITO KWA SERIKALI, MGAO WA MAJI DAR NA PWANI.

 ACT WAZALENDO YATOA USHAURI MZITO KWA SERIKALI, MGAO WA MAJI DAR NA PWANI.


Na Mwandishi wetu. 


Chama Cha Act Wazalendo kimeishauri serikali kuchukua mkopo nafuu wa muda mrefu wa shilingi trilioni 10 kutoka Benki za Maendeleo ili kutekeleza miradi ya maji ambayo imeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha ili kuondoa adha ya maji Kwa Wananchi.


Chama hicho pia kimeishauri serikali kutoa ruzuku Kwa Mamlaka za maji mjini na vijijini ili kuwezesha kupanua na kuboresha miundombinu ya maji katika maeneo yao Kwa kuzingatia mahitaji na Usawa kwani huduma ya maji ni muhimu na sio biashara.


Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa sekta ya Maji na Mazingira Ester Thomas wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia hali ya mgao wa maji inayoendelea katika mikoa ya Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.


Aidha amesema kuwa serikali hali ya upatikanaji wa maji Dar es salaam umekuwa wa kusuasua hivyo serikali iharajishe kutafuta fedha Kwa ajili ya kukamili miradi ya ujenzi wa bwawa la kidunda na mradi wa visima virefu 20 vya mpera na kimbiji sambamba nakushughulikia tatizo la upotevu wa maji linalotokana na uchakavu wa miundombinu.


Aidha amesema kuwa Kwa upande wa mikoani changamoto ya upatikanaji wa maji inachngia sana watu wa maeneo ya vinijini kukumbwa na dimbwi la umasikini kutokana nakutumia gharama kubwa katika kupata maji.


" Ndugu wa waandishi wa habari mfano Kijiji Cha gehandu huko hanang mkoani Manyara ambalo mwananchi ananua maji pipa Moja la Liga 200 Kwa shilingi elfu Saba, na familia Moja inahitaji angalau pipa Moja Kwa matumizi yakunibana hivyo mwananchi huyu atahitaji shilingi milioni 2.5 Kwa  mwaka Kwa ajili ya maji yakitumia yeye na familia yake" amesema Ester. 


Nakuongeza kuwa serikali inatakiwa kukamilisha miradi ya maji iliyokaa muda mrefu bila kukamilika na ile ambayo imeshindwa kutekelezwa kutokana uwepo wa ubadhilifu wa fedha za mradi huo.

Comments