KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA MCHANGO WA RAIS SAMIA, WIZARA KATIKA MABORESHO YA MICHEZO, SANAA

 

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA MCHANGO WA RAIS SAMIA, WIZARA KATIKA MABORESHO YA MICHEZO, SANAA


 



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imempongeza kwa mchango wake, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara Katika Maboresho ya Michezo, Sanaa.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo ameyasema haya Oktoba 25, 2022 baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya iliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa


"Waheshimiwa wajumbe wa Kamati sasa kwa hili naomba Kwa heshima nisimame na kusema kuwa mafanikio haya yote tunayoyapata kwenye mashindano ya Kombe la Dunia ni kutokana na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwenye michezo" amefafanua Mhe. Nyongo


Amemwomba Waziri Mchengerwa kuzileta timu za Taifa za soka za Serengeti girls na Tembo Warriors kuzileta bungeni ili zipewe pongezi mara baada ya kupambana na kuandika historia ya kuwa timu pekee kufika katika robo fainali za mashindano ya Kombe la Dunia. 

Comments