KINGLION KIBAHA FACTORY YASHIRIKI MAONESHO YA 3 YA BIASHARA PWANI.

 KINGLION KIBAHA FACTORY YASHIRIKI MAONESHO YA 3 YA BIASHARA PWANI.

Na mwandishi wetu, Kibaha Pwani. 

Kiwanda cha king lion Kibaha factory Kilichopo Kibaha mkoani Pwani kinashiriki katkka maonyesho ya 3 ya uwekezaji na  biashara mkoani Pwani ambapo kimewataka watanzania kutembelea Banda la kampuni hiyo na kujipatia bidhaa bora za pilipiki.


Mkurugenzi wa Kinglion Factory Ratnakar Wagh amemwambia Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete kuwa wamekuwa wakizalisha bidhaa bora za pikipiki hapa nchini ambazo zimeongeza idadi ya vijana waliojuajiri katika sekta ya usafirishaji. 


Ameongeza kuwa kupitia king lion kibaha factory wametengeneza ajira kwa vijana wa kitnzania ambo kuptia pikipiki na guta za  za king lion watanzania wameweza kujiajiri kwa kuzinunua na kupakia abiria.


Hata hivyo kiwanda hicho pia huzalisha bidhaa na nyingine ikiwemo mabati ya kisasa ya geji mbalimbali.


Pia. kampuni ya Kinglion Kibaha Factory katika maonyesho hayo yanayoendelea wilayani Kibaha wanauza pikipiki za kisasa kwa bei ya sh milioni 3.5 na nyingine milioni 2.5 huku pikipiki za matairi matatu (guta)zikiuzwa kwa shilingi milioni 5.7


Hata hivyo Kinglion Kibaha Factory imewasihi watanzania kuendelea kutumia bidhaa za Kinglion ikiwemo mabati na pikipiki sambamba na kutembelea Banda lao katika maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya Kibaha maili Moja mkoani Pwani. 

Comments