KIWANDA CHA RADDY FIBER TANZANIA LTD CHASHIRIKI MAONYESHO YA 3 YA UWEKEZAJI NA BIASHARA MKOA WA PWANI.
KIWANDA CHA RADDY FIBER TANZANIA LTD CHASHIRIKI MAONESHO YA 3 YA UWEKEZAJI NA BIASHARA MKOA WA PWANI.
Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa Raddy Fiber manufacturing Tanzania na Raddy Fiber solution ltd,Bw Nabil Hermina (aliyevaa tai nyekundu)akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la kampuni hiyo inayoshiriki katika maonesho ya 3 ya uwekezaji na biashara katika viwanja vya kibaha maili moja mkoani,Pwani
Na mwandishi wetu,Kibaha
Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing kinashiriki katika maonesho ya 3 ya uwekezaji na biashara ambayo yanafanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya kibaha,Maili moja mkoani Pwani.
Akizungumza katika banda hilo mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni hiyo Nabil Hermina amemwambia Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wameamua kushiriki maonyesho hayo ili kuwaonyesha watanzania ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho kilichopo Mkuranga,mkoani Pwani.
Kiwanda hicho kilizinduliwa rasmi mwezi Desemba 2021 na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo Kiwanda cha Raddy Fiber Manufacturing Ltd kilichopo Wilaya ya Mkuranga takriban kilomita 50 kusini mwa Dar es Salaam.
Amesema kuwa kiwanda hicho huzalisha kebo zenye ubora na vifaa vyake ili kuhakikisha watanzania wanapata bidhaa bora za vifaa vya umeme zinazozalishwa hapa hapa nchini.
Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha hadi kilometa 24,000 za fiber optic kwa mwaka na kimeajiri mamia ya watanzania na kukifanya kuwa cha tatu kwa ukubwa barani Afrika na cha kwanza Afrika Mashariki na Kati.
Kampuni ya Raddy Fiber Manufacturing Tanzania inajikita katika uzalishaji wa Kebo za Ubora wa Fiber Optic na Vifaa vyake. Bidhaa zetu mbalimbali hujumuisha matumizi yote ya ndani (FTTh Cables and Accessories) na matumizi ya nje (Cables ADSS, Micro cables na Armored Cable.
Comments