MKUTANO WA WADAU VYUO VYA UTALII WAFUNGULIWA DAR,WAZIRI AWASHAURI WAWEKEZAJI KUWEKEZA MIKOA YA KUSINI
MKUTANO WA WADAU VYUO VYA UTALII WAFUNGULIWA DAR,WAZIRI AWASHAURI WAWEKEZAJI KUWEKEZA MIKOA YA KUSINI
Waziri wa maliasiali na utalii,Balozi Dkt Pindi Chana akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) |
Waziri wa Mali Asili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana amewashauri wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya utalii hapa nchini kuwekeza katika mikoa ya Kusini kwa mwa Tanzania.
Dkt.Pindi Chana ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili uliowakutanisha wadau kutoka vyuo mbalimbali vya utalii nchini na serikali kujadili namna ya kuendeleza sekta ya utalii licha ya uwepo wa janga la Corona unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ulioandaliwa na chuo cha Taifa cha utalii.
Aidha amesema kubwa kwa sasa sekta ya utalii ni soko kubwa ambalo kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa hivyo jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika kuboresha Sekta hiyo.
Amesema kuwa serikali kupitia chuo cha Taifa cha utalii imekuwa ikitoa elimu bora kwa watumishi na wahudumu wa hoteli za kitalii na kuchangia katika uboreshaji wa sekta ya utalii kwa kuwafundisha ukarimu wahitimu wa chuo hicho pindi waingiapo makazini.
Kwa upande wake Kaim Afisa Mkuu wa Chuo cha Utalii Dkt. Florian Mtei amesema katika mkutano huo watapitia tafiti zilizofanywa na wataalamu kutokana nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini kuangalia changamoto zilizosababishwa na janga la Covid 19 na jinsi ya kukabiliana nazo ili kukuza sekta ya utalii.
Dkt Mtei amesema kuwa dhamira ya chuo cha TAIFA cha utalii kuandaa mkutano huo ni ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan ambaye ana dhamira ya dhati ya kuuza sekta ya utalii hapa nchini na duniani,pamoja na kukutana na wadau kujadili masuala mbalimbali ya utalii.
Sambamba na hayo amesema kuwa kupitia mkutano huo wataweza kuweka mikakati kama nchi kuangalia njia gani wanazoweza kufanya kuepukana na majanga kama Covid 19 yanayoisumbua Duniani.
Comments