NCCR Mageuzi yawataka wanasiasa kuwa na subira ripoti ya kikosi kazi,Yameongeza Rais Samia.

 

NCCR Mageuzi yawataka wanasiasa kuwa na subira ripoti ya kikosi kazi,Yameongeza Rais Samia.


Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema kinatambua kiu ya Watanzania kuwa na katiba mpya hivyo wanasiasa wasibeze kazi iliyofanywa na kikosi kazi cha Rais Samia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara Joseph Selesini amesema wameipongeza kikosi kazi kwa kuwasilisha maoni ya waliohojiwa na kumpongeza Rais Samia kwa kuyapokea.

“Ripoti ya Warioba ni bora kuliko zote ni sawa ila kikosi kazi ripoti yake kimechanganya pamoja na maoni ya ripoti ya Warioba na yeye pia alishiriki kutoa maoni kama kipo cha kuongeza au laa na pia ripoti ya kikosi kazi imeongezea na maoni ya tume huru ya uchaguzi” Amesema Selasini.

Aidha amesema kuwa ni vyema wakafanya uchambuzi wa yale ambayo yanaweza kutekelezwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na yafanyiwe kazi hivyo wanamuunga mkono Rais kusema apewe mda wa kutekeleza kazi 

Sambamba na hayo wamemuomba na kumshauri Rais Samia kuhakikisha kuwa mchakato wa ripoti hiyo haichelewi kwani mwaka 2024 kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka 2025 uchaguzi Mkuu ambapo wanategemea ripoti hiyo iwe imeshakamilika hususani Tume huru ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa kuhusu yale yaliyopo kwenye sheria na katiba ikiwemo mikutano ya siasa ifanyiwe kazi kwa haraka kwani kupitia mikutano hiyo itasaidia kutoa elimu kwa wananchi.

Amewataka wanasiasa wachambue ripot hiyo kwa maana ya kupeleka mawazo na mapendekezo zaidi badala ya kuchambua kwa kushambulia Rais na kikosi kazi chake ili kuboresha mshikamano kwa manufaa ya Taifa.

Kuhusu mgogoro wao ndani ya chama amesema wamefuata taratibu zote za kupata udhibitisho kupitia msajili wa vyama baada ya kufanya mkutano mkuu hivyo wao ndio wanaotambulika kisheria na atakayehusika kujitambulisha kuwa yeye ni kiongozi wa chama hicho atachukuliwa hatua pamoja na vyombo vitakavyomtamka kuwa ni kiongozi wa chama hicho.

Ameliomba Jeshi la polisi kujua kuwa maisha yao yapo rehani hivyo kufuatila taarifa zote wanazopeleka kwao na wao wako tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo.

Comments