SHIRIKA LA SENSE INTERNATIONAL TANZANIA LILIVYOWAINUA KIUCHUMI VIZIWI WASIOONA.

 SHIRIKA LA SENSE INTERNATIONAL TANZANIA LILIVYOWAINUA KIUCHUMI VIZIWI WASIOONA.


 





Na Thadei PrayGod,Dar es salaam.

Shirika lisilo la kiserikali la sense international Tanzania linalohudumia viziwi wasioona hapa nchini limesema litaendelea kutoa mafunzo na kuwasaidia vijana wenye ulemavu wa kutosikia na kutoona ili wafikie malengo yao kibiashara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkaazi wa Shirika hilo hapa nchini, Naomi Lugoe wakati Akizungumza na waandishi wa habari Kando ya mkutano wa tathmini ya mradi wa 'wezesha vijana' uliotekelezwa na Shirika hilo Kwa miezi minne ambapo vijana wenye ulemavu waliwezeshwa ili kufanya biashara na kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa vijana walionufaika na mradi huo ni wale ambao walimaliza shule za msingi katika shule maalum na baadaye kushindwa kuendelea na masomo kutokana na mifumo duni ya kielimu na ukosefu wa shule maalum zenye uwezo wa kuendelea kuwafundisha katika hatua za elimu ya juu kutokana na ulemavu wao.

"ndugu wanahabari kutokana na vijana hawa ambao hawasiki wala kuona kushindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na kukosekana Kwa shule zenye vifaa vitakavyowawezesha kupata elimu ya juu hivyo walivyomaliza elimu ya msingi Shirika la sense international Kwa kushirikiana na walimu wa hizi shule za viziwi wasioona na ofisi ya waziri mkuu, chama Cha wazazi na chama Cha viziwi wasioona tulikaa chini tukaangalia ni nini tunaweza tukafanya kuwasaidia wajikwamue kimaisha hivyo tukakaa nao na kubaini mahitaji yao kila mmoja,tukawapatia mafunzo ya biashara na utambuzi wa fedha na tukawaunganisha na viongozi wa serikali ambao ni maafisa biashara wanaoweza kuwasapoti" alisema bi Naomi.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mradi huo wa wezesha vijana ulianza na vijana hao wenye ulemavu 36 lakini waliofanya mradi huo ni 33 kutokana na wengine kufariki dunia Kwa sababu mbalimbali na wote 33 wamefanikiwa katika kuendesha biashara zao na wengine wamejenga nyumba, kuoa na kuolewa na kutengeneza familia zao kutokana na mradi huo wa wezesha vijana.

Kuhusu changamoto zinazowakabili viziwi wasioona ambao ni ulemavu adimu ni pamoja na gharama za mahitaji ya walemavu hao pamoja na jinsi ya kuwasiliana na wateja wao kutokana na kutumia lugha ya alama ya mguso jambo ambalo Shirika la sense international limewapa elimu juu ya kuendesha biashara zao Kwa kukabiliana na changamoto hizo. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama Cha viziwi wasioona Tanzania,David Kisaka amelishukuru Shirika la sense international Tanzania Kwa kushirikiana nao  Baga Kwa bega na kutatua changamoto zinazowakabili kupitia mradi wa wezesha vijana huku akiiomba serikali na jamii Kwa ujumla kuishirikisha kundi hilo katika mambo mbalimbali ya maendeleo kuanzia ngazi za chini. 

Amesema kuwa jamii imekuwa ikiwachukulia viziwi wasioona kama watu wenye matatizo ya akili jambo ambalo siyo la ukweli hivyo Kuna haja pia ya kutambuliwa rasmi hata kwenye mikopo ya asilimia 2 inatotolewa na halmashauri Kwa watu wenye ulemavu wa kutosikia na kutoona kwani kundi hilo limekuwa halipewi kipaumbele kutokana na changamoto za kimawasiliano tofauti na walemavu wengine.



Kwa upande wake Bi Mwanahamisi Samatta ambaye kijana wake aitwaye Hussein Samatta ana ulemavu wa kutosikia na kutoona amesema kuwa mradi wa wezesha vijana uliotekelezwa na Shirika la sense international Tanzania umemsaidia Kwa kiasi kikubwa kijana wake Kwa kumwezesha kufanya biashara ya duka na kujikwamua kiuchumi. 

Ameongeza pia mbali na kijana wake kuwezeshwa na Shirika hilo pia alipata mkopo wa asilimia 2 unaotolewa na halmashauri na hatimaye kununua bajaji ambayo pia anaitumia kuendesha maisha yake licha ya kukabiliwa na changamoto kutokana na kutopata madereva waaminifu. 

.




Naye Bi Mariam Nkumbwa ambaye ni afisa kutoka idara ya afya ustawi wa jamii na lishe pamoja na makundi maalum katika ofisi ya Rais, Tamisemi amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwawezesha watu wenye ulemavu na Kwa sasa wameandaa muongozo wa utambuzi Kwa watu wenye ulemavu. 

Amesema kundi hilo limekuwa na changamoto lukuki kutokana na mahitaji yao kuwa maalum hivyo serikali imeandaa mpango maalum Kwa ajili ya kuwatambua na kuwawezesha kiuchumi. 


Comments