Skip to main content

SIKU YA POSTA DUNIANI: MFUMO WA KIDIGITALI WA HUDUMA YA POSTA KIGANJANI WAZINDULIWA TANZANIA, IMO STEMPU YA USHIRIKIANO KATI YAKE NA OMAN.

 

SIKU YA POSTA DUNIANI: MFUMO WA KIDIGITALI WA HUDUMA YA POSTA KIGANJANI WAZINDULIWA TANZANIA, IMO STEMPU YA USHIRIKIANO KATI YAKE NA OMAN. 






Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Posta Duniani jijini Dar es Salaam.


Posta Master Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbondo akizungumza katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Posta Duniani jijini Dar es Salaam.

Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine ulimwenguni katika kuadhimishaa siku ya posta duniani,WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amezindua mfumo wa Kidigitali wa Posta Kiganjani utakao msaidia mteja kupata huduma kutoka Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa njia ya mtandao.

Katika uzinduzi huo wa kihistoria ambao haukuishia tu kuzindu mfumo huo pekee,Bali ulienda sambamba na uzinduzi wa Stempu ya ushirikiano baina ya Tanzania na Nchi ya Oman katika masuala ya Utalii ambayo itakuwa chachu ya mashirikiano baina ya mataifa hayo mawili. 

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Oktoba 9, 2022 jijini Dar es Salaam uliokwenda sambamba na Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Posta Duniani, Waziri Nape amesema Mfumo wa Posta Kiganjani utawarahisihshia wateja kupata huduma za Shirika la Posta Tanzania bila ulazima wa kufika ofisini.

"Niwapongeza Shirika la Posta kwa kuanzisha mfumo huu wa Kidigitali, hii inamanisha kwamba mtakuwa mmewafikia Watanzania wengi. Kwa takwimu tu ni kwamba Tanzania kuna simu milioni 58, hivyo kila Mtanzania anatumia simu. Watanzania milioni 37 wanatumia simu kama njia ya manunuzi. Hivyo kupeleka huduma kiganjani umechukua watu milioni 37," amesema Waziri Nape.

Hivyo Waziri Nape ameeleza kuwa anaamini Shirika la Posta limejipanga kuhakikisha linatoa huduma bora kuendana na mabadiliko ya teknolojia, kwamba Serikali imejipanga kuhakikisha watoa huduma za posta watoe huduma bila kufika ofisini.

"Niwatake watoa huduma za Posta, kutumia Anuani za Makazi ili kufikisha huduma zao kwa wananchi kwa urahisi," ameelekeza Waziri Nape.

Waziri Nape pia amepongeza kwa kufikia makubaliano na kuzindua Stempu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Oman kwani nchi hizi zina historia nzuri.

Kwa upande wake Posta Master Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbondo akizungumzia Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Posta Duniani ambayo huadhimishwa Oktoba 9 ya kila mwaka amesema kauli mbiu ya mwaka hii ni "Posta kwa Kila Mtu,".
 
Mbondo amebeinisha maeneo tisa yanayolifanya Shirika la Posta kuendena na kauli biu hiyo ambayo yanalifanya Shirika kumgusa kila Mtanzania.

Maeneo hayo ameyataja kuwa ni katika nyanja ya Usalama. Katika suala la usalama amesema wamekuwa wakishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuzuia uingizwaji wa silaha haramu pamoja na madawa ya kulevya nchini.

Kwamba wamekuwa wakifanikisha kukamatwa kwa wahusika na kuchukuliwa hatua.

Mengine ni maeneo ya Biashara ambapo wamefanikisha wafanyabiashara kufanya biashara ndani na nje ya nchi kupitia duka mtandao. Eneo la Elimu, amesema katika eneo hilo wamekuwa wakisaidia wanafunzi katika kufikisha fomu za mikopo kwa Bodi ya Mikopo Tanzania.

Mbondo maeneo mengine aliyotaja ni Sekta ya Afya, kushirikiana na Serikali katika utoaji huduma wa pamoja ikiwemo huduma za NIDA, Eneo la Kiuchumi, Eneo la Usafirishaji, Utalii na TEHAMA.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali Yohana Mabongo amesema watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa matumizi ya kidigitali kwa biashara endelevu.

Comments