Tanzania yawa nchi ya kwanza Afrika kuwa wenyeji wa Shindano la Dunia la Urembo, Utanashati na Mitindo kwa viziwi duniani.

 Tanzania yawa nchi ya kwanza  Afrika kuwa wenyeji wa Shindano la Dunia  la Urembo, Utanashati na Mitindo kwa viziwi duniani.







Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika na ya 12 duniani kuwa mwenyeji Mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani baada  ya mashindano hayo kufanyika mara 12 baada ya kuanzishwa kwake.


Kauli hiyo imetolewa  katika mkutano wa Waandishi wa Habari  jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas na Rais wa Mashindano ya Urembo na Utanashati kwa Viziwi Duniani, Bonita Lee kutoka nchini Marekani.


Shindano hilo litafanyika leo JNICC Dar ea Salaam ambapo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Mhe. Doroth Gwajima Waziri wa Jinsia,  Wanawake na Makundi maalum Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.   Mohamed Mchengerwa ambaye atakuwa mgeni maalum.


Dkt. Abbas amefafanua kuwa  Serikali imewapa  zawadi  washindi wote wa shindano hilo la kidunia  na  viongozi kutembelea mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro Oktoba 31,2022  baada ya kumalizika kwa shindano hilo kesho ikiwa ni mwendelezo wa Royal Tour  aliyoiasisi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.


Amesema tukio hilo litarushwa  na mitandao  mbalimbali duniani  ikiwa na pamoja na kituo cha televisheni cha AZAM  ambacho kitarusha mbashara kupitia kipindi chake cha Sinema zet  kuanzia majira ya saa mbili usiku. 


Pia amesema  katika  tukio hili   maalum itawajumuisha  waalikwa zaidi ya 1000 ambapo filamu ya Royal Tour  iliyochezwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaanza kuonyeshwa  ili watu waweze jinsi Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na   vivutio mbalimbali vya utalii.


Aidha, ameongeza  kwamba   burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa  miziki mbalimbali zitaoneshwa  kwa washiriki na ameomba  washiriki kuwa tayari kupokea matokeo kutoka kwa majaji  kwani  hadi kufika  hapa tayari wote  ni washindi.

Comments