Skip to main content

VIJANA WABUNIFU KUKUTANISHWA NA SAHARA SPARKS JIJINI DAR ES SALAAM

 VIJANA WABUNIFU KUKUTANISHWA NA SAHARA SPARKS JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mtendaji wa Shara Ventures Jumanne Mtambalike akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Meneja Mradi wa Funguo ulioko chini ya UNDP Joseph Manirakiza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu, Dar es salaam. 

Ili kuhakikisha sekta bunifu inaendelea kujua hapa nchini KAMPUNI Sahara Sparks kuanzia leo Oktoba 18, itaendesha makongamano mbalimbali ya  vijana wabunifu yatakayofanyika katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya Shara Sparks, Mkurugenzi Mtendaji wa Shara Ventures Jumanne Mtambalike amesema kongamano hilo litajadili namna gani ubunifu, teknolojia na ujasiriamali vinaweza kuwa ni chachu ya kuchangia maendeleo ya Tanzania.

"Sahara Ventures ni Kampuni tanzu ya Shara Sparks ambayo inaandaa hili kongamano la vijana wabubifu lakini velevile ambao wanajiuhusisha na masuala ya teknolojia na ujasiriamali," amesema Mtambalike na kuongeza,

"Kwa kipindi cha takribani miaka saba (7) Sahara Ventures wamekuwa wakiandaa hili tukio la Sahara Sparks kama Jukwaa ambalo linaleta pamoja vijana wenye mawazo yakiubunifu, lakini pia na watunga sera kuweza kujadili mnagani ubunifu, teknolojia na ujasiriamali vinaweza vikawa ni chachu ya kuchangia maendeleo ya Tanzania kama Taifa,"

Amesema wamekuwa wakifanya mijandala mbalimbali ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni "Potantial Unleashed" kwamba namna gani wanaweza kufungua uwezo wa vijana kupitia teknolojia, ubunifu pamoja na ujasiriamali.

"Na kutakuwa na mijadala mbalimbali ambayo itaanza kesho tarehe 18 mpaka tarehe 21, 2022. Tutakuwa tunaangalia kwenye nyanja mbalimbali namna gani teknolojia na ubunifu vinatumika kwenye elimu, Afya, nishati na ajira," amesema Mtambalike.

Hivyo amesema wanategemea kufanya mijadala mingi sambamba na kuvumbua fursa nyingi kwa vijana kwa kushirikiana na wadau ambao ni pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mradi wa Funguo na Clouds Media Group.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu amesema wao kama wasimamizi wa masuala ya ubunifu, wanakila sababu ya kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kuonekana, kubadilishana mawazo na kuweza kutangaza biashara zao.

"Ukweli ni kwamba vijana wana mawazo mazuri, kwahiyo kuwa na Jukwaa kama hili ni sehemu inayowapa fursa vijana kujitambua, kuwa pamoja na kuwa wabunifu lakini wanajua soko lina taka nini," amesema na kuongeza,

"Kwahiyo hapa vijana wanakutanishwa na kujifunza na kukutana pia na wawekezaji wa kuweza kukuza mawazo yao. Kwasababu siku zote serikali kazi yake ni kuweka mazingira wezeshi. Serikali sio mfanyabiashara,".

Amesema Sahara Sparks inasaidia kuwajengea vijana uwezo wa kujua lugha ya kutumia ambayo mwekezaji anaitaka.

Comments