"WAANDISHI WA HABARI NI SEHEMU YA JAMII,WANAPASWA NAO PIA KUTETEA MASLAHI YAO"BALILE

 "WAANDISHI WA HABARI NI SEHEMU YA JAMII,WANAPASWA NAO PIA KUTETEA MASLAHI YAO"BALILE

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile akizungumza alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi katika Semina hiyo ilichofanyika leo Oktoba 20,2022 Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer akizungumza wakati alipokuwa akifungua rasmi Semina hiyo iliyowakutanisha wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya habari Jijini Dar es Salaam.


Washiriki wa Kikao hicho ambao ni wahariri na waandishi wa habari waliofika kuhudhuria kikao  hicho.


Mhariri wahabari wa Clouds TV na Clouds FM Joyce Shembe (kulia) akiwa na Mhariri wa habari wa BBC Swahili wakifuatilia hotuba ya Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer katika kikao hicho.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anitha Mendoza (kushoto) akiwa na Ofisa kutoka katika Taasisi hiyo Elizabeth Chanzi katika kikao hicho.

Mwenyekiti Mstaafu wa TEF Theophil Makunga akizungumza katika kikao hicho alipokuwa akitoa neno la shukrani mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kufungua kikao hicho Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa TEF Bakari Machumu (kushoto) katika mkutano huo.



Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutambua kuwa nao ni sehemu ya jamii ambayo wamekuwa wakiandika juu ya changamoto za jamii kwa kuitetea hiyo hivyo nao wanapaswa pia kutetea maslahi na haki zao kama sehemu ya jamii hiyo.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na jukwaa hilo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu utetezi wa mabadiliko ya Sheria ya vyombo vya habari.

Balile amesema kuwa waandishi wa habari wa nchi za Afrika hufundishwa kutetea maslahi ya jamii kwa kiasi kikubwa hatua ambayo wanasahau kama nao ni sehemu ya jamii hiyo na wana haki pia ya kutetea maslahi na haki zao na taaluma yao kwa ujumla.

“Kuna baadhi ya taasisi zinasema wanatetea haki za waandishi lakini wao sio waandishi na hawazijui changamoto za waandishi ndio maana tukasema tuanze kutetea haki na maslahi yetu wenyewe,” amesema Balile.

Aidha Balile amezungumzia vifungu vya sheria ya habari na kueleza wapo kwenye mchakato wa kuona namna ambavyo Bunge litapitia upya sheria hizo hususani ni zile zinazoleta vikwazo kwa waandishi wa habari ili vifanyiwe marekebisho.

Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer akizungumza alipokuwa akifungua semina hiyo amelipongeza Jukwaa la Wahariri (TEF) kwa kuwa na  programu za kuwajengea uwezo wanahabari ili wafanye kazi kwa weledi na kwamba ubalozi huo uko tayari kushirikiana jukwaa hilo. 



(NA:

Comments