WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI JANGWANI WATAKIWA KUTUMIA VYEMA MITANDAO.
WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI JANGWANI WATAKIWA KUTUMIA VYEMA MITANDAO.



Na Thadei PrayGod,Dar es salaam.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ya jijini Dar es salaam wametakiwa kuwa makini na vitu wanavyoposti katika mitandao ya kijamii ili wasije jaribu hatma za maisha yao hapo baadaye kwa kuweka picha zisizofaa mitandaoni.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa masuala ya usalama mtandaoni Eng Steven Wangwe alipokuwa akizungumza na wanafunzi hao wakati maafisa mbalimbali wa wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari walipotembelea na kutoa elimu ya masuala ya mbalimbali ya matumizi ya mitandao ikiwa wizara hiyo inaadhimisha mwezi wa usalama wa mtandao.
Eng Wangwe amesema kuwa wanafunzi hasa wa kike wamekuwa ni waathirika wakubwa wa matukio hasa ya unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying)hivyo ni wakati wao wa kubadili matumizi ya mitandao ikiwemo ya Facebook,Instagram,Twitter,TikTok na mitandao mingine kwa kupost vitu vinavyoendana na maadili ambavyo haviwezi kuyaharibu maisha yao.
Aidha mhandisi Wangwe amesema kuwa licha ya kutoa elimu shule ya sekondari ya Wasichana Jangwani ,Wizara hiyo intarajia kutoa elimu hiyo maeneo mbalimbali nchini ili kuwezesha wanafunzi na jamii kwa jumla kuacha kutumia vibaya mitandao hiyo kwa kuchapisha jumbe zisizofaa pamoja na kuposti picha ambazo hazina maadili.
"Wizara ya habari,Mawasiliano na Teknolojia ya habari tunatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,na usalama wa mtandao (cyber security)mwezi mmoja tunautumia kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ili kusaidia kuzingatia maadili kwenye mitandao"amesema Mhandisi Wangwe.
Kwa upande wake mwalimu wa shule ya sekondari ya Wasichana Jangwani Salum Kilipamwambu amesema kuwa elimu hiyo inasaidia wanafunzi kujitambua nakuwezesha kujikita kwenye masomo nakuachana na tabia ya kuposti mambo yasiyofaa mtandaoni.
Aidha amesema kuwa Wizara hiyo imefanya jambo jema kutoa elimu shuleni hapo kwani atua hiyo itawafanya wanafunzi kutumia vizuri mitandao ya kijamii, nakusaidia wanafunzi kutumia mitandao hiyo kwa manufaa yao ya masomo.
"Somo la teknolojia ya habari na Mwasailiano(TEHAMA) shuleni linafundishwa lakini halipewi kipaumbele katika ufundishwaji ,hivyo tunaiomba serikali itilie mkazo somo hili muhimu kwa wanafunzi ili wajue mapema matumizi sahihi ya mtandao"amesema Mwalimu Kilipamwambu.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliyopewa elimu juu ya matumizi usahihi ya mitandao akiwemo Anna Ngowi ambaye anasoma kidato cha 6 shuleni hapo amesema hatua ya Wizara ya habari kutoa elimu hiyo ni yakuungwa mkono kwani imewapa elimu nzuri juu ya jinsi gani wataepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii,huku Neema Matinde ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha 5 aliipongeza wizara kwa elimu hiyo ambayo imekuja wakati muafaka ambao mitandao ya kijamii inatumiwa kama sehemu ya maisha.
"Kwa sisi wanafunzi tunashukuru kwa kupewa elimu hii,na tumejifunza ni vitu gani vya kuposti na visivyo vya kupost mitandaoni ili visitudhalilishe na kupelekea kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying)hivyo nawaomba vijana wenzangu hasa wanafunzi watumie vyema mitandao"amesema Neema Matilda ambaye ni wanafunzi wa kidato cha 5 shuleni hapo.


Comments