WESE WAJA NA MPANGO KABAMBE UNAOMWEZESHA DEREVA KUPATA MAFUTA NA KULIPIA BAADAYE.

 

WESE WAJA NA MPANGO KABAMBE UNAOMWEZESHA DEREVA KUPATA MAFUTA NA KULIPIA BAADAYE.



Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe leo amezindua mpango 'bidhaa' wa kampuni ya WESE ambayo itaawawezesha kutoa Suluhu ya madereva wadogo wa kibiashara kununua mafuta sasa na kulipa baadaye.


DC Gondwe amesema kuwa kupitia teknolojia hiyo ya wese vijana wa Jiji la Dar es salaam hasa wilaya yake ya Kinondoni watanufaika pakubwa na mpango huo Kwa kuwawezesha kupata bidhaa ya mafuta na Kisha kuilipia baadaye.

Hata hivyo ameopongeza mpango huo Kwa kusema kuwa utaketa mapinduzi makubwa katika teknolojia hapa nchini na kuinua uchumi wa madereva wa vyombo vya usafiri wa kibiashara ikiwemo bodaboda na bajaji

Mkurugenzi Mwanzilishi wa kampuni hiyo Fransis Ekeng amesema lengo la kuja na mpango huo wa kununua mafuta na kulipa baadaye ni ili kuleta mabadiliko katika maisha ya madereva wa usafiri wa kibiashara kote Tanzania na kote Afrika.

Ameongeza kuwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania ni mojawapo ya waajiri wakubwa kwani uchumi hujengwa Kwa kiasi kikubwa na sekta pia ya uchukuzi.


“ndugu wanahabari madereva wadogo wa kibiashara wanakabiliwa na hali dunia ya maisha, huku takwimu zikionyeaha kuwa asilimia 95 ya madereva nchini Tanzania hawamiliki vyombo vya usafiri wanavyoviendesha na mara nyingi wamekuwa wakiwajibika katika matengenezo ya vyombo hivyo pia tasnia ya fedha imekuwa haiwaamini madereva kwa kuwapa mikopo midogo ili kusimamia ustawi wa maisha yao ya kila siku ndiyo maana WESE tukaja na mpango huu wa kuwawezesha kupata mafuta sasa na kulipa baadaye” amesema Ekeng. 


Amesema madereva wanaotaraajia kunufaika na mpango huo wa kupata mafuta na kulipa baadaye watapaswa kuipakua applikesheni ya WESE, kujisajili na Kisha Kuanza kufurahia mpango huo utakaoinua uchumi wa madereva nchini. 

Aidha ameongeza kuwa WESE itakuwa jukwaa la kwanza la kiteknolojia hapa nchini ambalo linaendeshwa na vijana wa kitanzania wenye hakimiliki nchini Tanzania na itapelekwa pia katika mataifa mengine ya Afrika. 


Naye mkuu wa kitengo Cha malipo benki ya Equity ambao ni washirika wa kampuni hiyo amesema kuwa benki hiyo itakuwa ikipokea fedha ambazo zitalipwa na madereva na kuzifikisha Kwa wahusika ‘wenye vituo vya mafuta’ ambapo pia amesema kuwa teknolojia ambayo kampuni ya WESE imekuja nayo ni nzuri na itakuwa na manufaa Kwa madereva wa vyombo vya usafiri vya kibiashara. 


Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Engen ambao vituo vyao vya mafuta’ vitakuwa vikitoa huduma hiyo ya kununua mafuta na kulipa baadaye Kwa madereva wa vyombo vya kibiashara amesema wameamua kuungana na Wese Kwa kuhakikisha wanatatua changamoto za madereva kupitia vituo vyao vya Engen kote nchini. 

Comments