CHINA DASHENG BANK YAFUNGUA TAWI JIPYA KARIAKOO.

 CHINA DASHENG BANK YAFUNGUA TAWI JIPYA KARIAKOO.


Na mwandishi wetu,
Dar es salaam.

Benki ya China Dasheng leo imezindua tawi jipya la benki hiyo katika mtaa wa Lumumba na Aggrey uliopo Kariakoo, Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi wa tawi hilo ni katika kuendeleza biashara kati ya Tanzania na China Kwa nchi za Afrika na litatoa huduma zote za kibenki katika tawi hilo.

Aidha kupitia benki hiyo wafanyabiashara wa kitanzania hasa wa masoko ya Kariakoo ambao huagiza biashara zao kutoka nchini China watapata urahisi wa kufanya biashara zao kupitia benki hiyo ya China Dasheng kupitia tawi lake hilo jipya. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo,Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Chenga Ji ameishukuru serikali ya Tanzania Kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara Kwa kuipa leseni benki hiyo Kuanza kufanya kazi hapa nchini mwezi November, 2022.

Ameongeza kuwa benki hiyo pia imeongeza nafasi za ajira kwa kuajiri watanzania kufanya kazi katika benki hiyo na hivyo kuwakwamua kiuchumi.

Aidha ameongeza kuwa benki hiyo itatoa huduma Kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa na itakuwa ni chachu ya kukuza uchumi baina ya nchi ya Tanzania na China kupitia wafanyabiashara.

Rais wa chemba ya wafanyabiashara wa kariakoo Juma SHI Kwa wafanyabiashara wa kichina ameishukuru benki hiyo Kwa kufungua tawi lake karibu na wafanyabiashara wa kariakoo likiwa ni tawi la kwanza la benki ya China na litasaidia kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kitanzania na China na kurahisisha biashara baina ya Tanzani na China. 

Aidha amewaomba watanzania kutumia benki hiyo yenye viashiria vya China kuitumia benki hiyo katika kufanya biashara zao kwani ni benki ambayo ndani ya miaka minne tu Tanzania,tayari imeonyesha mwanga wa mafanikio katika uwekezaji.

Comments