Skip to main content

JESHI LA POLISI KUTEKETEZA SILAHA HARAMU JIJINI DAR ES SALAAM

 

JESHI LA POLISI KUTEKETEZA SILAHA HARAMU JIJINI DAR ES SALAAM


Jeshi la Polisi nchini linapenda kuwataarifu kuwa kutakuwa na zoezi la uteketezaji wa silaha haramu ambazo zilisalimishwa katika kampeni maalumu iliyofanyika nchi nzima kuanzia tarehe 01.09.2022 hadi tarehe 31.10.2022 iliyokuwa ikiongozwa na kaulimbiu isemayo "Silaha haramu sasa basi, salimisha kwa hiari,".

Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 05.09.2022 katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, baada ya tangazo la serikali la msamaha wa usalimishaji silaha kwa hiari namba 537 la tarehe 26.08.2022 ambalo lilieleza kuwa yeyote anaemiliki silaha kinyume cha sheria anatakiwa kuisalimisha katika kipindi cha tarehe 1 septemba hadi 31 octoba 2022, na yeyote atakayefanya hivyo hatashitakiwa.

Kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya mwezi wa Usalimishaji wa Silaha haramu Afrika, baada ya zoezi la Usalimishaji silaha kukamilika zinatakiwa kuteketezwa kwa moto hadharani na wananchi washuhudie ikifanyika hivyo.


Hivyo basi, nawakilisha kuwa zoezi hilo la uteketezaji silaha haramu litafanyika siku ya Jumanne tarehe 22.11.2022 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya shabaha vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ vilivyopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (MB).


Jeshi la Polisi linapenda kuwaalika na kuwaomba Viongozi wa Serikali za mitaa na wananchi hasa wanaoishi maeneo ya Kunduchi kuhudhuria ili kujionea mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kampeni hiyo.


Imetolewa na: 
David A. Misime - SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodo¬ma, Tanzania.


Comments