KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UINGEREZA LAFANYIKA DAR.

KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UINGEREZA LAFANYIKA DAR. 

 


Dar es salaam,Kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na Uingereza limekutanisha wafanyabiashara zaidi ya 100 yakiwepo makampuni na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 30 kutoka nchini Uingereza. 


Akizungumza kuhusu kongamano Naibu Katibu Mkuu, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, anayeshughulikia uwekezaji, Ally Gugu amesema masuala ya kisera, sheria na changamoto za biashara na uwekezaji yatajadiliwa.


Aidha amesema kuwa kongamano hilo pia litakuwa ni fursa ya kukuza mashirikiano ya biashara baina ya Tanzania na UK. 


"Ili kuimarisha ushirikiano na uhusiano tumeona tuanzishe kongamano hili ili kujadili masuala ya kisera, fursa na changamoto wanazokitana nazo wafanyabiashara ili zifikishwe kwa mamlaka husika na kutafutwa ufumbuzi," amesema.


Katika Kongamano hilo ambalo linafanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini hapa, majadiliano yatakayofanyika yatahusisha taasisi za umma za Uingereza na Tanzania, kadhalika wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uingereza.


Mwisho wa kongamano hilo, amesema mataifa hayo yatajadili kwa pamoja kilichojadiliwa na kutatua kila changamoto.


Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, amesema pamoja na nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), nchi zinazoendelea zitanufaika na fursa zilizopo


Aidha ameongeza kuwa ifikapo mwaka 2023 UINGEREZA inatarajia kutekeleza mpango maalumu kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vya biashara ikiwemo kodi chechefu ili kuzifanya nchi hizo kuweza kufikia soko lake.


Akizungumzia umuhimu wa kuwa, Jukwaa hilo pamoja na mambo mengine ambayo yatajadiliwa katika kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili lakini litatoa fursa kwa wafanyabiashara na kuwawezesha kutambua fursa za biashara na uwekezaji zilizopo.




Aidha, amesema kuwa licha ya Taifa hilo kujiondoa katika umoja wa Ulaya (EU) haitaathiri ushirikiano wao na mataifa ya Afrika kwani watahakikisha wanaondoa kodi ili kuwezesha bidhaa za Tanzania kuingia katika soko shindani.



Comments