MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MZEE ZAIDI AFARIKI DUNIA
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MZEE ZAIDI AFARIKI DUNIA
Priscilla Sitienei amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.MWANAFUNZI mkubwa zaidi wa elimu ya msingi nchini Kenya, Priscilla Sitienei amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.
Sitienei alikuwa maarufu kwa jina la Gogo ambalo kwa lugha ya asili ya kabila la Kalenjin linamaanisha ‘bibi’.
Mjukuu
wa Sitienei, Sammy Chepsiror amelieleza gazeti la The Standard la
nchini humo kuwa ‘Gogo’ amefariki dunia akiwa katika hali ya utulivu
mbele ya baadhi ya wanafamilia.
Hadithi
yake ya kujiunga na elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 94
iliwavutia watengeneza filamu wa Ufaransa waliotengeneza filamu ya Gogo,
ambayo ilimpa fursa “Gogo” kukutana na mke wa rais wa Ufaransa,
Brigette Macron.
Priscilla Sitienei akiwa na wanafunzi wenzake enzi za uhai wake
Priscilla Sitienei akiwa na wanafunzi wenzake enzi za uhai wakeMmoja
wa waandishi wa filamu hiyo, Patrick Pessis ametuma salamu za
rambirambi kufuatia msiba huo akiandika katika ukurasa wa Twitter
“ujumbe kuhusu elimu kwa wasichana unaendelea kubaki”.
Gogo
Sitienei alijiunga na shule ya watoto ya Vision Preparatory School
akijiunga na darasa la wanafunzi ambao ni sawa na vilembwe wake
alipoamua kurejea shule akiwa na miaka 90 baada ya kufanya kazi ya
ukunga wa jadi kwa zaidi ya miongo miwili.
Sitienei
hakufanikiwa kujiunga na shule alipokuwa mdogo lakini serikali ya Kenya
ilipoamua kuweka unafuu wa gharama za elimu ya msingi mwaka 2003
ilimhamasisha Gogo na wazee wengine kurejea darasani.
Mwaka
2015 Gogo aliiambia BBC kuwa analenga kuwahamasisha watu wazima kurejea
shule “Wananiambia wao ni wakubwa [na hawawezi kurudi shuleni kusoma]”
nitawajibu, “Mimi ni mzee [zaidi yao] na ninasoma darasani hivyo ni
lazima warudi kusoma”. Alinukuliwa na BBC.


Comments