NAIBU WAZIRI MWAKIBETE AIPONGEZA KAMPUNI YA GF TRUCKS & EQUIPMENT KWA UWEKEZAJI MITAMBO YA MADINI.

 NAIBU WAZIRI MWAKIBETE AIPONGEZA KAMPUNI YA GF TRUCKS & EQUIPMENT KWA UWEKEZAJI MITAMBO YA MADINI.



Afisa mkuu wa Biashara na Masoko wa GF Trucks & Equipment Limited, Bwana Salman Karmali akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) mheshimiwa Atupele Mwakibetemara baada ya kutembelea na kuijionea namna GF Truck & Equipment Limited inavyofanya kazi zake katika hafla ya kuanzishwa rasmi Chama chama cha Wamiliki wa Matipa na Mitambo Tanzania (TTMOA) uliyofanyika katika hotel ya serena jijini Dar es salaam.





Na Thadei PrayGod 
Dar es salaam.
Naibu waziri wizara ya ujenzi na uchukuzi,Atupe Mwakibete amepongeza jitihada zinazofanywa na kampuni ya Gf Trucks &Equipment kwa jitihada inazofanya katika uuzaji na usambazaji wa mitambo ya kisasa ya ikiwemo ya migodini.

Naibu waziri Mwakibete ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua moja ya mtambo wa migodini XCMG unaouzwa na kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa Chama cha wamiliki wa matipa na mitambo tanzania (TTMOA) kilichozinduliwa katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Amesema Kampuni ya Gf Trucks &Equipment imefanya jitihada kubwa katika sekta ya madini kwa kuhakikisha wachimbaji wanapata mitambo bora ya uchimbaji na malori ya mizigo.

Awali akitoa maelezo mbele ya naibu waziri huyo,Afisa mkuu wa biashara na masoko wa kampuni hiyo,Salman Karmali alisema mitambo inayouzwa na kampuni ya Gf Trucks Equipments ambao huuza na kusambaza mitambo na malori ya mizigo ya FAW ni yenye kiwango cha juu na ya uhakika katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Karmali aliongeza kuwa kwa sasa kampuni hiyo huagiza mitambo hiyo kutoka nje ya nchi lakini wanatarajia  kuanza kuunganisha mitambo ya shughuli za migodini hapa hapa nchini kupitia tawi la kampuni hiyo lililopo wilayani Kibaha,mkoani Pwani.

"Mheshimiwa naibu waziri sisi kama GF Trucks ambao tuna miaka 15 toka tuanze biashara hapa nchini mbali na kuagiza mitambo kutoka nje na kuiuza kwa wachimbaji madini na makampuni ya uchimbaji pia tunatarajia kuanza kuiunganisha mitambo hiyo hapa nchini ikiwa ni Sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza maendeleo na uchumi wa viwanda"alisema Afisa huyo mkuu wa biashara na masoko.

Aliongeza kuwa kampuni ya Gf Trucks & Equipment imekuwa ikitoa waranti ya mpaka masaa elfu tatu kwa mitambo inayouzwa na kampuni hiyo hapa n unaouchini. 

Kampuni ya Gf Trucks & Equipment huuza mitambo ya shuguli mbalimbi ikiwemo za migodini ya XCMG pamoja na magari ya mizigo ya FAW.


Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa GF Trucks & Equipment Limited, bwana Salman Karmali akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Chama Cha Wamiliki wa Matipa na Mitambo Tanzania (TTMOA) uliyofanyika katika hotel ya serena jijini Dar es salaam
Moja ya mtambo aina ya XCMG unakuzwa na kampuni ya Gf Trucks &Equipment

Comments