TAMASHA LA THE BIG PRAISE CONCERT LAFANYIKA,WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI.
TAMASHA LA THE BIG PRAISE CONCERT LAFANYIKA,WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI.

Na Thadei Praygod,Dar es salaam
wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na muziki wa injili hapa nchini wametakiwa kujitokeza ili kudhamini matamasha ya Muziki huo na kuifikisha injili katika maeneo mbalimbali kupitia muziki.Hayo yamesemwa na mwandaaji na mratibu (Mbeba maono) wa tamasha la muziki wa injili la The big Praise Concert, Johnson Jackson alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa tamasha hilo lililofanyika katika kanisa la FPCT lililopo Kurasini jijini humo.
Bw Johnson amesema kuwa tamasha hilo la muziki wa injili lenye lengo la kumtukuza na kumsifu MUNGU linafanyika ikiwa ni msimu wake wa tano tangu kuanzishwa kwake lakini changamoto ya uhaba wa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa matamasha hayo imekuwa ikiwakabili kama waandaaji.
Ameongeza kuwa kama mwandaaji wa tamasha hilo anawakaribisha wadhamini mbalimbali ili kushirikiana nao katika uandaaji wa matamasha kwa kutoa fedha zitakazowezesha uandaaji mzima wa Tamasha ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa rasilimali watu pamoja na kuwalipa wasanii ambao wanashiriki kutoa huduma katika matamasha ya The big Praise Concert.
"nadhani ndugu waandishi wa habari mmeona jinsi tamasha letu lilivyofanyika na tumefanikiwa kwa kiasi fulani japo changamoto ya kifedha katika uandaaji wa matamasha ya injili ni kubwa sana lakini tutakapopata fedha za kutosha tutafanya matamasha haya hata mara mbili kwa mwaka katika maeneo tofauti na milango yetu kwa wadhamini iko wazi"amesema Johnson.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo Apostle Christine Mbelwa amempongeza kwa kazi anayofanya na moyo wa utayari alio nao hivyo yuko tayari kumsaidia.
Amesema kuwa tamasha hilo limekuwa lakufana na Mungu ameonekana kupitia shuhuda mbalimbali za vijana waliopiga hatua kupitia tamasha hilo.
Tamasha la The Big Praise Concert limehudhuriwa na waimbaji mbalimbali ambapo pia kumetolewa vyeti vya kutambua mchango mkubwa wa baadhi ya wadau katika kuhakikisha kuwa wanafanikisha tamasha hilo.





Comments