MAONESHO YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA YAZINDULIWA DAR, TANTRADE YAASWA KUENDELEZA BIASHARA.

 MAONESHO YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA YAZINDULIWA DAR, TANTRADE YAASWA KUENDELEZA BIASHARA.

Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika katika uwanja wa kimataifa wa maonesho ya biashara sabasaba kuanzia desembar 3 Hadi 9 mwaka huu Jijini Dar es salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tan Trade Bi  Latifa Khamis. 



Na Thadei PrayGod, Dar es salaam

Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban ametoa rai Kwa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania,TanTrade kuongeza kasi katika utekelezaji majukumu ya kusimamia na kukuza biashara nchini.

Waziri huyo ametoa wito huo leo Desemba 4,2022 Jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua rasmi maonesho ya Saba ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika katika uwanja wa kimataifa wa maonesho ya biashara (sabasaba)kuanzia Desemba 3 mpaka 9 mwaka huu.

Ameopongeza hatua ya TanTrade kuendelea kuratibu maonesho hayo ambayo yamekuwa chachu ya kutangaza bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.

"Nimepata fursa ya kutembelea mabanda ya washiriki na nimejionea mwenyewe bidhaa zilizopo changamoto ni chache lakini ni vyema kuweza kuzifanyia marekebisho kwa kukaa pamoja ili kuweza kufikia lengo la kuthamini vya kwetu"amesema


Aidha amevitaka viwanda hapa nchini kuongeza ubora wa bidhaa wanazozalisha na Kasi ya uzalishaji ili kukuza uchumi na kuongeza kuwa sekta ya viwanda imechangia katika kutoa ajira nchini hivyo serikali itaendelea kukuza sekta hiyo. 

Amesema serikali imejipanga kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji Kwa kuondoa changamoto katika mazingira ya uwekezaji na biashara ambayo yatachangia ongezeko la viwanda vya ndani ikiwemo upatikanaji wa umeme wa uhakika katika viwanda hapa nchini. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tan Trade Bi  Latifa Khamis amesema idadi ya washiriki wa maonesho ya Saba ya viwanda imeongezeka ukilinganisha na mwaka Jana.

 "Mwaka huu jumla ya washiriki 502 wameweza kushiriki maonyesho haya wakati mwaka Jana walishiriki 121,kila siku ya maonyesho kutakuwa na vikao na wafanyabiashara ili kuweza kujadili changamoto zao katika uboreshaji wa bidhaa,"amesema Latifa.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni 'nunua bidhaa za Tanzania Jenga Tanzania' lengo kubwa ni kuboresha bidhaa.

Amesema pamoja na kuandaa maonyesho mbalimbali lakini pia wameanzisha app ya Tan Trade biashara lengo ni kuwawezesha wakulima kujua Bei ya bidhaa akiwa nyumbani kwake kwa kutumia sm yeyote haijalishi ni kitochi au simu janja (android)

MAONESHO ya bidhaa za viwanda vya Tanzania Kwa mwaka huu yanafanyika Kwa mara ya 7 hapa nchini tangu kuanziahwa kwake na kuratibiwa na mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania TanTrade. 


Comments