Skip to main content

MAONYESHO YA SEKTA YA AFYA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA DESEMBA 14 JIJINI DAR ES SALAAM.

 

 MAONYESHO YA SEKTA YA AFYA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA DESEMBA 14 JIJINI DAR ES SALAAM. 






NA MWANDISHI WETU
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa maonesho makubwa ya sekta ya dawa na huduma za afya kutoka kwa wadau na wataalam wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 7, 2022 jijini Dar es Salaam Afisa Masoko wa Vegvoraus Thomas James amesema maonyesho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia Desemba 14 hadi 16 mwaka huu.

James amesema maonyesho hayo yatawakutanisha wazalishaji, wauzaji wa jumla, wafanyabiashara na wasambazaji wa sekta ya uchunguzi wa dawa, hospitali na watoa ushauri wenye ushawishi mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Maonyesho haya yameidhinishwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) ikiwa na dhumuni la kutaka Watanzania wapate fursa ya kujifunza l, kushirikiana na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zitakazoshiriki,” amesema James na kuongeza,

“Tunaamini hii ni fursa kubwa kwa wadau wa Sekta ya Afya nchini,” amesema James.

James ameyashukuru mashirika binafsi na ya kiserikali yaliyokubali kishirikiana nao ikiwemo Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA), Confederation of Tanzania Industries (CTI) na Tanzania Exporters Association (TANEXA) na mashirika mengine.

Maonyesho hayo yanatarajia kuleta pamoja wabobezi zaidi ya 90 kutoka Jumuiya ya Sekta ya Dawa na Afya kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka TWCC Cresensia amesema maonyesho haya ni muhimu kwa nchi ya Tanzania kwani  washiriki zaidi ya 90 kutoka mataifa mbalimbali ambao wataonyesha bidhaa zao.

“Pia itaongeza ugunduzi na ubunifu wa bidhaa mpya na matukio katika sekta ya afya,”inakutanisha amesema Cresensia

Comments