TAMASHA LA UIMBAJI NA MIUJIZA KUANZA LEO BCIC, MBEZI BEACH

 TAMASHA LA UIMBAJI NA MIUJIZA KUANZA LEO BCIC, MBEZI BEACH





Na Thadei PrayGod, Dar es salaam

Tamasha kubwa la uimbaji na miujiza Tanzania linaanza leo Jijini Dar es salaam ambapo muinjilisti wa kimataifa kutoka nchini Canada Dkt Peter Youngreen atahubiri. 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mwenyeji wa tamasha hilo Askofu Sylvester Gamanywa amesema kuwa tamasha hilo linafanyika katika ukumbi wa kanisa la BCIC Mbezi Beach Jogoo linaanza leo Ijumaa, Desember 2,2022 na kuhitimishwa jumapili ya Desember 4,2022 kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 1 usiku. 

Amesema Tanzania imepata neema kubwa ya kutembelewa na mhubiri huyo wa kimataifa na itapokea baraka na miujiza.

Ameongeza kupitia tamasha hilo linaloanza leo watanzania watapata fursa ya kupokea baraka,miujiza kubarikiwa na kumjua Mungu aliye hai na Yesu Kristo. 

Kwa upande wake muinjilisti huyo wa kimataifa Dkt Peter Youngreen ameishukuru kwa mapokezi aliyoyapata hapa nchini na kusisitiza kuwa kupitia tamasha hilo watanzania watamwona Mungu kupitia miujiza yake na uponyaji. 

Amesema kuwa utajiri mkubwa kuliko wote duniani ni watu hivyo watu wanapaswa kumjua mwenyezi Mungu Ili awaponye na kuwafanyia miujiza na uponyaji. 


"Nataka kuongea na Afrika na wakati huu wa kufunga mwaka nataka niwaambie vijana wa bara hili wamtambue Yesu Kristo Kwa kuwa nyakati tulizonazo sasa katika dunia siyo njema hivyo kama vijana watamjua Yesu Kristo na kumuamini watapokea miujiza wao na Taifa Kwa ujumla "amesema mwinjilisti huyo wa kimataifa 

Amewataka watanzania kuwapeleka watu mbalimbali wenye mahitaji wakiwemo walemavu na waliokata tamaa ili kwenda kupokea uponyaji na miujiza.

"niliona watu wengi waliokata tamaa lakini baadaye kupitia neno la Mungu wakapokea miujiza hivyo nawakaribisha sana watu wote hapa Wapo Mission Center waje kupokea miujiza" ameongeza Dkt Peter Youngreen 

Amesema maombi hayo ya siku tatu yatakuwa ni muhimu katika kuiombea jamii na Taifa Kwa ujumla.

Comments