MAENDELEO BANK PLC YATANGAZA KUPATA FAIDA ZAIDI YA MARA MBILI MWAKA 2022,YAWATAJA MACHINGA KATIKA FAIDA HIYO.

  MAENDELEO BANK PLC YATANGAZA KUPATA FAIDA ZAIDI YA MARA MBILI MWAKA 2022,YAWATAJA MACHINGA KATIKA FAIDA HIYO.


Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC, Dkt Ibrahim Mwangalaba Akizungumza na waandishi wa habari leo January 30,2023 katika makao makuu ya benki hiyo Jijini Dar es salaam wakati benki hiyo ikitangaza kupata faida mara 8 mfululizo. 

Na Thadei PrayGod, Dar es salaam

Benki ya Maendeleo hapa nchini Maendeleo Benki (PLC) imetoa ripoti ya ufanisi wa utendaji kazi wake ambapo kwa mwaka 2022 imefanikiwa kupata faida zaidi ya mara mbili kutoka milioni 587 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 1.3 kwa mwaka 2022.


Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt. Ibrahim Mwangalaba amesema kuingezeka kwa faida hiyo kumechangiwa na kuongezeka kwa ukuaji wa jumla wa mapato kwa asilimia 22 mwaka hadi mwaka kutoka shilingi za kitanzania 12.8 bilioni hadi 15.6 bilioni mwaka 2022.


“Mapato halisi yaliongezeka kwa asilimia 31 kutoka shilingi bilioni 7.6 mwaka 2021 hadi shilingi za kitanzania 9.9 bilioni mwaka 2022, pia tuna biashara ya mikopo kutokana na kuimarika kwa hali ya uchumi, tumeboresha ubora wa vitabu vya mkopo kutoka mikopo chechefu ya asilimia 13 mwaka 2021 hadi asilimia 5.2 mwaka 2022 jambo ambalo limechangia pakubwa benki kuwa na mapato mazuri” Amesema Dkt. Mwangalaba.


Aidha ameongez kuwa amana za wateja ziliongezeka kwa adilimia 11 kutoka shilingi bilioni 70 kwa mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 77 mwaka 2022 wakati mikopo na malipo ya awsli kwa wateja yaliongezeka kwa asilimia 5 kutoka shilingi bilioni 57 hadi bilioni 60 mwaka 2022.


Dkt Mwangalaba amesema benki ya maendeleo inamtaji wakutosha na wanatazamia kufanya kazi nchini kote ikiwemo kuongezeka tawi moja katika eneo la Mbagala kabla ya mwezi wa nne, kuanzisha huduma za kimtandao,(Internet Benking) pamoja na kuanzisha mfumo wa ulipaji ada ambao utapeleka taarifa papo hapo kwenye shule husika pindi mzazi atakapolipa ada kupitia benki hiyo na kuondoa usumbufu wa kupeleka risiti shuleni.


Kuhusu mikopo Dkt Mwangalaba amesema kwa mwaka 2022 benki hiyo iliwakopesha wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga 2500 kwa kuwapatia mikopo iliyofikia shilingi bilioni 3 ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliochangia kuongezeka kwa faida ya benki hiyo.


Hatahivyo  amesema kwa mwaka 2023 benki hiyo imeweka mikakati ya kuwafikia wafanyabiashara wadogo zaidi ya elfu tano, vijana pamoja na makundi ya wanawake wajasiriamali kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu.


Comments