MahafaliFURAHIKA: WAZAZI WASHAURIWA KURUDI KWENYE CHIMBUKO LA MALEZI YA WATOTO/VIJANA

 #MahafaliFURAHIKA: WAZAZI WASHAURIWA KURUDI KWENYE CHIMBUKO LA MALEZI YA WATOTO/VIJANA


Naibu katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama Cha mapinduzi CCM,Daniel George Akizungumza katika mahafali ya Chuo Cha FURAHIKA yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Buguruni Malapa Jijini Dar es salaam jana.
Naibu katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama Cha mapinduzi CCM, Daniel George Akizungumza na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Dar es salaam,Bi Khadija Ally Said katika sherehe za mahafali ya Chuo Cha FURAHIKA Jijini Dar es salaam Jana. 
Mkuu wa chuo Cha FURAHIKA,Edward Msuya akifuatilia jambo wakati wa sherehe za mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika Jana Jijini Dar es salaam 

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam


Wito umetolewa Kwa wazazi na walezi hapa nchini kurudi kwenye chimbuko la malezi yenye kuzingatia utamaduni wetu ili kuzalisha watoto, vijana na Taifa lenye weledi katika malezi.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na naibu katibu mkuu bara wa jumuiya ya umoja wa wazazi wa chama Cha mapinduzi CCM  Daniel George, alipokuwa akizungumza katika mahafali ya Chuo Cha Furahika yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo katika eneo la Buguruni, Malapa Jijini humo. 

Amesema kuwa kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili Kwa miaka ya hivi karibuni jambo ambalo lina hangiwa Kwa kiasi kikubwa na suala la malezi hivyo kama wazazi na walezi wa kitanzania watawalea watoto wao Kwa kufuata misingi ya utamaduni na kuachana na malezi ya kuiga kwenye mitandao jambo hilo litachochea kurejelesha tabaia njema na maadili mema miongoni mwa watoto na vijana hapa nchini kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kabla ya uwepo wa mitandao na ukuaji wa teknolojia.

Ameongeza kuwa jumuiya ya wazazi wa chama Cha mapinduzi CCM itaendelea kusisitiza suala la malezi na kuhakikisha kunakuwepo na malezi bora ambayo hayatoliabu Taifa Kwa kuzalisha vijana wasio na maadili.

Kuhusu mahafali ya Chuo Cha Furahika .. amewataka wahitimu hao wakazitumie taaluma zao walizopata kujikwamua kiuchumi ikiwemo kujiajiri Kwa kuondokana na fikra kuwa ni lazima kupata kazi baada ya kumaliza Chuo kwani soko la ajira haliwezi kuchukua wahitimu wote wanaomaliza masomio Kwa wakati Mmoja.

Aidha naibu katibu mkuu huyo wa jumuiya ya wazazi CCM bara,ameahidi kulifanyia kazi suala la upungufu wa wanafunzi na chakula katika Chuo hicho Kwa kuzielekeza idara za jumuiya hiyo kuandaa mazingira ya kupeleka chakula chuoni hapo kama ilivyoombwa na mkuu wa chuo hicho ambacho hutoa elimu bure.

Hata hivyo amekipongeza Chuo Cha Furahika Kwa kupata eneo la zaidi ya ekari 3 kwa ajili ya kujenga majengo yake yatakayomilikiwa na Chuo hicho.

Awali Akizungumza katika mahafali hayo mkuu wa chuo Cha Furahika, Edward Msuya amesema Chuo hicho kinajiendesha kupitia fedha za ufadhili ambapo mwanafunzi huchangia shilingi 50,000 pekee na kusomea kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo na kupata huduma ya chakula bila malipo.

Ameongeza kuwa Chuo hicho kinaendelea kupanuka katika baadhi ya kozi ikiwemo kozi za ufundi, lugha ya kiingereza na kifaransa na hutoa fursa Kwa wanafunzi waliomaliza darasa la Saba na wale wa kidato Cha nne ambao walishindwa kuendelea na elimu ya sekondari ambapo hupata kozi fupi zinazoanzia miezi mitatu na kuendelea. 

Aidha amesema Chuo hicho kinachotambulika na Veta na chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kinatarajia Kuzindua program ya utengenezaji wa pikipiki ambayo inatarajia Kuanza mwezi April mwaka huu ambapo mfadhili wa chuo hicho anatarajia kuleta mitambo maalum ya kisasa ya utengenezaji wa pikipiki. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa chama Cha mapinduzi CCM, Mkoa wa Dar es salaam Bi Khadija Ally Said amewasihi waende kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho Kwa kutangaza mema yake hali itakayochochea kuongezeka Kwa idadi ya wanafunzi.

Sambamba na hayo Bi Khadija amewataka wahitimu hao kuwa makini na malezi ya siku hizi ambayo yana changamoto lukuki za kimalezi kutokana na ukuaji wa teknolojia. 

Comments