KONGAMANO KUBWA LA KIBIASHARA DAR,LAHUDHURIWA NA WADAU MBALIMBALI
MICO HALAL YAFANYA KONGAMANO KUBWA LA KIBIASHARA DAR,LAHUDHURIWA NA WADAU MBALIMBALI
NA Mwandishi wetu.
Katikaa kuboresha mazingira ya kubiashata hapa nchini kampuni ya Kimataifa ya Ithibati (viwango) Mico imefanya kongamano la kwanza la kibiashara jijini Dar es Salaam lenye lengo la kubainisha, kutoa elimu na kuweka wazi masoko ya bidhaa mbalimbali.
kongamano hilo limefanyika jijini Dar es Salaam ambapo Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Skeikh Hamid Jongo ameipongeza Halal kwa kuandaa kongamano hilo na kuongeza kuwa litaleta manufaa makubwa nchini.
Sheikh Jongo ameeleza kwamba uwepo wa Taasisi ya Halal nchini ni jambo jema kwani imekuwa ni kiu ya muda mrefu kwa wafanyabiashara na Serikali.
Hivyo Taasisi hii itasaidia kutoa uthibati kwa bidhaa mbalimbali hivyo kusaidia kupenya katika masoko ya ndani na nje na kuchangia pato la Taifa.
“Pengine tumekuwa tukikosa soko la kuuza bidhaa, hivyo wafanyabiashara bidhaa zao zitathibitishwa kupitia Halal na hivyo kuongeza mapato kwa kwa Serikali,” amesema Sheikh Jongo.
Sheikh Jongo amebainisha kwamba licha ya hayo, ni kwamba itasaidia kupatikana kwa bidhaa bora kama vile za chakula, nguo na kadhalika kwa ajili ya afya njema za wateja.
Ameeleza kuwa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linaunga mkono na kupongeza kwa jambo hilo kwani litasaidia Mtanzania kula chakula safi, mavazi safi na hivyo kuwa na maisha mazuri.
Kwamba wafanyabiashara wa Tanzania wamekuwa wakienda nchi zingine kwa ajili ya kufata ithibati ya bidhaa zao hivyo Halal itawarahisishia kupata ithibati ndani ya nchi.
“Kwa kupatikana kwa kampuni ya Halal itakuwa rahisi kwa wafanyabiashara kupata ithibati na kufanya biashara ndani na nje,” ameongeza Sheikh Jongo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TanTrade Latifa Khamis amesema kwamba soko la Halal limekwenda kimataifa.
Hivyo kupitia Halal wafanyabiashara watasaidiwa kujua bidhaa halali na zisizo halali ili kuweza kuhimili soko la ndani na nje.
“Hivyo ili wafanyabiashara waweze kufanya vizuri wanatakiwa kijua Halal ni nini, naomba waitumie sana Halal kwani itawapatia ithibati ya bidhaa zao,” amesema Latifa.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Mico Halal Muhamed Juma amesema kwamba kongamano hilo ni la kwanza na lengo lake ni kubainisha, kuelimisha na kuweka wazi masoko.
Kwamba kongamano hilo limekaribisha wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara lengo kujifunza na kupata ufahamu kuhusu Halal. la adhabu ya kikatili waliyoipata wanafunzi wawili wa shule ya msingi Majanja wilayani Kyerwa mkoani Kagera kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
Hatua ya shirika hilo inafuatia kusambaa kwa video fupi katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini ikimwonysha mkuu huyo wa shule Isaya Benjamin akiwacharaza bakora kwenye nyayo za miguu wanafunzi wawili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo januari 26,2023 mkurugenzi mtendaji wa shirika la Haki elimu,Dkt John Kalage amesema kuwa kitendo hicho kinakiuka siyo tu haki za watoto bali pia ni kinyume na maadili ya kazi ya ualimu na malezi bora kwa wanafunzi.
Dkt Kalage ameongeza kuwa shirika hilo linaipongeza serikali kupitia waziri wa elimu,sayansi na teknolojia Prof Adolf Mkenda na uongozi wa mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka na za awali dhidi ya mwalimu aliyehusika na ukatili huo ikiwa ni pamoja na kumvua nafasi yake ya ualimu mkuu,kumsimamisha kazi na kuunda tume ya kuchunguza tukio hilo ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe.
Aidha Dkt Kalage ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya hali ya ukatili nchini iliyotolewa na jeshi la polisi,visa vya ukatili kwa watoto viliongezeka kwa asilimia 25.9% kutoka visa 5,803 vilivyoripotiwa mwaka 2015 hadi visa 7,388 mwaka 2020.
"katika utafiti uliofanywa na shirika la Haki elimu mwaka 2020,takribani asilimia 87.9 ya watoto wa shule waliripoti kufanyiwa ukatili wa kimwili huku asilimia 90 kati ya hao walisema ukatili wa kimwili waliofanyiwa ulitokana na adhabu za viboko zinazotolewa shuleni,huku asilimia 54.9 ya watoto walisema walimu wao na walezi wanatumia kupiga ngumi na makofi kama Sehemu ya adhabu'alisema Dkt Kalage.
Kutokana na matukio hayo shirika hilo pia limeishauri serikali kuchukua hatua ambazo zitakomesha kabisa matumizi ya adhabu za viboko shuleni na kuhimiza adhabu chaya/mbadala ambazo siyo za kikatili.
"ni rai yetu vipengele vya sheria ya elimu ya mwaka 1978,mwongozo wa elimu juu ya adhabu za viboko wa mwaka 2002 na sheria ya mtoto ya mwaka 2009,vipitiwe upya ili kukataza kabisa matumizi ya viboko shuleni na kuzuia adhabu nyingine ambazo zinaweza kutoa mwanya wa ukatili wa watoto kufanyika"aliongeza Dkt Kalage.
Sambamba na hayo shirika hilo limetoa mapendekezo 9 kwa serikali ikiwa ni pamoja na program ya uanzishwaji wa shule salama 600 nchi nzima ambayo inalenga kuondoa ukatili wa namna yoyote na kuzifanya shule kuwa Sehemu salama na rafiki pa kujifunzia ambayo imetangazwa hivi karibuni na serikali,ilenge shule zote 18,000 nchini ikiwemo shule za msingi 12,000 na sekondari 5000.
Mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja na serikali kuweka mipango endelevu ya kuimarisha mifumo rasmi ya ulinzi na usalama kwa watoto ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa madawati ya ulinzi na usalama kwa watoto shuleni pamoja na wadau kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi,wazazi na jamii ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto katika maeneo ya shule,nyumbani,nyumba za ibada na maeneo yote ambayo watoto hukusanyika.
Hata hivyo Dkt Kalage ameongeza kuwa,Haki elimu inapendekeza serikali kuchukua hatua dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya ukatili wa dhidi ya watoto ili kuvikomesha ndani na nje ya shule pamoja na kuhuisha miiko na maadili ya walimu ili kuwagusa hata walimu ambao wanashindwa kuzuia matendo ya ukatili kwa watoto yanayofanywa na walimu wenzao mashuleni kama ambavyo imeonekana katika video ya tukio la mwalimu mkuu kupitia video iliyosambaa mitandaoni.
- Get link
- X
- Other Apps




Comments