MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI,(UVCCM)ILALA MOHAMED BALHABOU ASHIRIKI ZOEZI LA KUFANYA USAFI,KUTOA MISAADA ZAHANATI YA VINGUNGUTI
MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI (UVCCM)ILALA MOHAMED BALHABOU ASHIRIKI ZOEZI LA KUFANYA USAFI,KUTOA MSAADA ZAHANATI VINGUNGUTI
![]() |
| Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Uvccm wilaya ya Ilala, Mohamed Balhabou (aliyevaa kofia)akiwa na baadhi ya vijana wa kata ya Vingunguti mara baada ya kufanya usafi sambamba na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika wodi ya wazazi,zahanati ya Vingunguti leo Januari 1,2023 |


Na Thadei Praygod,Dar es salaam.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji,umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Ilala Mohamed Ally Balhabou amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo ya halmashauri kwani serikali imedhamiria kuwakwamua vijana kiuchumi.
Mjumbe huyo ameyasema hayo Hii leo alipotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya Vingunguti iliyopo wilayani Ilala, Jijini Dar es salaam ikiwemo mradi wa machinjio ya Vingunguti katika eneo la mabucha ya kisasa ya kuhifadhia na kukatia nyama,daraja la juu katika mradi wa SGR pamoja na zahanati ya Vingunguti ambapo ametoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika zahanati hiyo,pamoja na kushuhudia bonanza la michezo.
Akiwa ameambatana na vijana wa Chama cha mapinduzi wa kata ya Vingunguti na viongozi wao,Bw Balhabou alifanya usafi kwa kusafisha maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni ya kuogea na kufulia ya watoto pamoja na taulo za watoto wachanga (pamprers) kwa akina mama waliojifungua katika zahanati hiyo.
Aidha amesema kuwa vijana wanapaswa kuhakikisha wanaomba mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa vikundi mbalimbali ikiwemo vya vijana ili kufanya biashara.
"nimeshazungumza na vijana kuhusu asilimia 10 za halmashauri ambayo kati yake vijana hupewa asilimia 4 ya mikopo hiyo,kinamama asilimia 4 na walemavu asilimia 2 kwa hiyo nimewahamasisha waichangamkie kwani haina riba hivyo wakachukue kwa vikundi vyao kwa ajili ya kujiendeleza"amesema Bw Balhabou.
Kuhusu miradi aliyoitembelea amesema wao kama vijana wameridhishwa na jinsi miradi hiyo inavyotekelezwa kupitia ilanin ya chama cha mapinduzi CCM,ambayo pia imetoa fursa za ajira kwa vijana wa kata hiyo na kuwahakikishia kuwa atazifikisha changamoto za vijana Sehemu sahihi ili zitatuliwe.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa zoezi hilo la usafi mwenyekiti wa umoja wa vijana kata ya Vingunguti Mikidadi Kyando amesema hatua ya kufanya usafi katika zahanati na kuwasaidia wagonjwa katika wodi ya wazazi,zahanati ya Vingunguti ni kuwafanya vijana wawe na moyo wa kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya umma na hatua ya kutoa misaada ni sehemu ya kumsemea Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi anazofanya katika kuleta maendeleo huku akiwataka wananchi kuwapuuza wapinga maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali za MITAA kata ya Vingunguti Sharifu Abdala Mbulu ambaye pia ni mwenyeti wa serikali ya mtaa wa Vingunguti amesema wameamua kufanya usafi, kutoa misaada na baadaye kufanya bonanza la mchezo wa Mpira wa miguu ili kuwakusanya vijana pamoja, kuibua vipaji kupitia michezo kama ilani ya CCM inavyosema.



Comments