VIONGOZI DINI TUSIPIGANE VITA,WENYEWE KWA WENYEWE:PROPHET PHILBERT PASCHAL
VIONGOZI DINI TUSIPIGANE VITA,WENYEWE KWA WENYEWE:PROPHET PHILBERT PASCHAL

Na PrayGod Thadei,Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na mtumwa wa Mungu,Nabii Filbert Paschal wa kanisa la la Bwana Yesu kwa mataifa yote lililopo Kinyerezi jijini Dar es salaam alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kanisani hapo kuhusu masuala mbalimbali ya kidini na kijamii.
Nabii Filbert amesema kuwa kumekuwepo tabia ya baadhi ya viongozi wa kidini na kiroho kunyoosheana vidole na mifarakano ya wenyewe kwa wenyewe jambo ambalo halina umuhimu katika mafundisho ya kuwajenga kiroho waumini wa madhehebu yao.
"Ndugu waandishi wa habari watanzania wengi sana wanamtafuta Mungu na kitu nachokiomba kwa viongozi wa dini na kiroho hasa kwa sisi wakristo,kama bosi wetu ni mmoja makanisa ni kama idara au wizara na huwezi kusikia wizara ya kilimo inapigana vita na wizara ya fedha au wizara ya afya inakinzana na wizara ya elimu haipo,Kwani wote wanajenga nyumba moja (Tanzania)hivyo hata sisi viongozi wa dini inatakiwa tuwe wamoja kwa kuwajenga watu wamjue kristo na tukipigana vita na kusemana vibaya na wote ni wamoja tunafanya ukristo udorore na kuwafanya watu wengi wamwache kristo"alisema nabii Filbert
Aidha aliongeza kuwa vita ya wachungaji katika makanisa mbalimbali inasababisha pia watu (waumini)kumwona kristo hafai hivyo amewaomba viongozi hao kuitana na kuzungumza pale inapotokea kuna mmoja amekosea na si kusemana vibaya kwa kushambuliana hadharani bali waelekezane ili kazi ya Mungu isonge mbele.
Kuhusu matukio ya ukatili na mmomonyoko wa maadili hapa nchini nabii Filbert alisema kuwa jamii inatakiwa kuyatafuta maarifa na kuwa na ufahamu kwani matukio hayo husababishwa na kukosa maarifa na ufahamu.
Aliongeza kuwa endapo jamii itajengewa maarifa ya maisha kupitia mchango wa viongozi wa dini na kujengwa kimaadili hatua hiyo itapunguza mawazo ya watu kufanya vitendo vya kikatili hasa dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo ubakaji.
"haya mambo tunayoyaona ya ukatili wa kijinsia,kubaka watoto na ukosefu wa maadili yanatokea kwa sababu watu wamekosa maarifa na ufahamu hivyo nawashauri viongozi wa dini na serikali kwa ujumla kuwekeza zaidi kwa kuwajengea watu ufahamu na maarifa kwani watu huangamia kwa kukosa maarifa na hata mmomonyoko wa maadili hutokea kwa watu kukosa maarifa na kukosa maarifa simaanishi digrii bali ni maarifa ya maisha"aliongeza nabii Filbert Paschal.
Aidha alisema kuwa kanisa la Bwana Yesu kwa mataifa yote litaendelea kuwajenga waumini wake kwa kuhubiri neno la Mungu na kuwapa watu maarifa katika jamii hatua itakayochangia jamii kuwa na maadili mema na kuondokana na matukio ya ukatili.
Aidha alisema kuwa kanisà hilo pia limekuwa likitoa misaada kwa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo madereva wa bodaboda,mama lishe ,wajasiriamali,mashule na makundi mengine yenye uhitaji kwa kile ambacho Mungu amewajalia kupitia taasisi ya kanisa ijulikanayo kama Prophet Philbert Foundation.


Comments