Skip to main content

DC KOMBA AWATULIZA WAFANYABIASHARA SOKO LA SIMU 2000

 

DC KOMBA AWATULIZA WAFANYABIASHARA SOKO LA SIMU 2000






Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashim Komba akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Simu 2000.

NA MWANDISHI WETY
MKUU wa Wilaya ya Ubungo Hashim Komba amawataka wafanyabiashara a wa la Simu 2000 kuwa watulivu wakati ukitafutwa mfumo mzuri wa kuboresha soko hilo.

Ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakilalamikia Manisapaa ya Ubungo kutaka kuwapatia mikataba ili wawe wanalipa kodi.

DC Komba amesema kwamba anasimamia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia biashara wafanyabiashara wadogowadogo.

Amesema kwamba dhimira ya Serikali  kwa wafanyabiashara hao ni njema kwani inania ya kuboresha mazingira ya biashara.

“Maboresho ya soko ni lazima, na dhamira ya Serikali ni wafanyabiashara kufanya biashara katika mazingira mazuri,” amesema DC Komba.

Hivyo ametumia fursa hiyo kusema kwamba watakaa na kamati ya maboresho ya siko hilo na kuja na njia ya sahihi ya kufanikisha maboresho kwa maslahi ya wafanyabiashara na Halmashauri.

Katika hatua nyingine amemuagiza Meneja wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa maji machafu yanayotiririka kwenye vibanda vya wafanyabiashara, kadhalika kuketa gari la kunyonya maki machafu kwenye choo.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho ya Soko hilo Mussa Andile alimweleza Mkuu wa Wilaya hiy9 chabgamoto wanazopitia

Comments