ELIMU BILA MALIPO NI MOJA YA MAFANIKIO MAKUBWA YA CCM NDANI YA MIAKA 46:MOHAMMED BALHABOU

 ELIMU BILA MALIPO NI MOJA YA MAFANIKIO MAKUBWA YA CCM NDANI YA MIAKA 46:MOHAMMED BALHABOU

Na Thadei Praygod,Dar es salaam
Chama cha mapinduzi CCM,leo kinasheherekea miaka 46 tangu kuanzishwa kwake mnamo Februari 5,1977 

Sherehe za kuadhimisha miaka 46 ya chama hicho zimefanyika katika mikoa mbalimbali hapa nchini huku kukiwa na shamra shamra lukuki huku Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume wakitajwa kama waanzilishi wa chama hicho ambacho kinaliongoza Taifa la Tanzaani hadi sasa.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam maadhimisho ya chama hicho yamefanyiKa katika viwanja vya mnazi mmoja huku mgeni Rasmi katika sherehe za maadhimisho hayo kwa mkoa huo zikiongozwa na makamo wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Ilala Bw Mohamed Ally Balhabou amesema suala la elimu bure bila malipo ni moja ya mafanikio makubwa ya chama hicho katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora.

Balhabou amesema kuwa suala la elimu limekuwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho ambapo kwa sasa elimu hutolewa bure kuanzia shule ya awali,msingi,sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Aidha amepongeza hatua ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa ada katika shule zote za umma za sekondari nchini kuanzia kidato cha tano na sita mapema mwaka jana jambo ambalo limekuwa na muitikio mkubwa kwa mustakabali wa elimu hapa nchini.

Hata hivyo Bw Mohamed Ally Balhabou ameongeza kuwa katika miaka 46 ya chama cha Mapinduzi CCM,hapa nchini pia suala la afya limepewa kipaumbele kikubwa ambapo vituo mbalimbali vya kutoa huduma ya afya kuanzia ngazi za mitaa,kata hadi Taifa vimeongezeka hali ambayo imechangia pakubwa katika utoaji na upatikanaji wa uhakika wa huduma za afya kwa watanzania.

"ndugu wanahabari katika Hii miaka 46 ya CCM hasa katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita tumeona hospitali zimeongezwa na siyo tu kwa Mkoa wa Dar es salaam bali kwa Tanzania nzima na hata katika suala la umeme tumeona changamoto za upatikanaji wa umeme zinakwenda kumalizika zote muda siyo mrefu"alisema Mohamed Balhabou.

Ameongeza kuwa mafanikio mengine ya chama hicho hasa kwa Mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na mradi wa mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) ambapo tayari awamu ya kwanza ya miradi huo kuanzia Mbezi,Kimara,Morocco,Gerezani na Kivukoni unafanya kazi huku miradi huo wa awamu ya pili ukiendelea kumalizika kuanzia Mbagala,Gerezani na Kivukoni ambapo utakuwa na manufaa makubwa katika sekta ya usafirishaji katika jiji hilo la kibiashara hapa nchini.

"Sisi kama vijana miradi yote Hii iliyofanywa na serikali inayoongozwa na CCM na inatupa taswira nzuri ya kumsemea vizuri Rais wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba anafanya kazi nzuri kwani kwa muda mfupi ambao amekaa madarakani amefanya makubwa"aliongeza Balhabou

Aidha amewaasa vijana wa Tanzania kuendelea kulipigania Taifa kwa kufanya kazi na kujishughulisha ambapo pia amewashauri kujiunga vikundi na kuomba mikopo kupitia halamashauri zao wanazotoka ili kujijenga kiuchumi ambapo mikopo hiyo ya asilimia 10 hutolewa kwa makundi mbalimbali ya kijamii,ikiwa ni asilimia 4 kwa vijana,asilimia 4 kwa wanawake na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu.

Comments