KAMPUNI YA VIJANA REAL ESTATE YAMPA SHAVU LA UBALOZI, MAULID KITENGE, YAUTANGAZA MRADI MKUBWA WA VIWANJA BAGAMOYO.

 KAMPUNI YA VIJANA REAL ESTATE YAMPA SHAVU LA UBALOZI, MAULID KITENGE, YAUTANGAZA MRADI MKUBWA WA VIWANJA BAGAMOYO. 




Na Thadei PrayGod, Dar es salaam
Kampuni ya Vijana Real Estate imemtangaza mchambuzi wa soka na mtangazaji maarufu wa vipindi vya michezo kutoka E-fm, Maulid Kitenge kama balozi wa kampuni hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kutangazwa kama balozi wa kampuni hiyo inayohusika na uuzaji wa viwanja, Maulid Kitenge ameishukuru Vijana Real estates Kwa kumchagua huku akiahidi kuitumia nafasi hiyo katika kuhamasisha watanzania kuwekeza katika sekta ya ardhi.

Hata hivyo mtangazaji huyo maarufu hapa nchini ameutangaza mradi wa viwanja uliopo katika eneo la Kilomo, Bagamoyo Mkoani Pwani kama mradi mkubwa ambao ataanza nao kuwatangazia watanzania fursa zake za kumiliki viwanja vya makazi na biashara.

Amesema kuwa mradi wa Viwanja wa Kilomo upo sehemu nzuri kwani Bagamoyo sasa inakwenda kuchangamka na kukua kiuchumi kufuatia serikali kutangaza Kuanza Kwa mradi mpya wa  Ujenzi wa bandari ya kisasa Bagamoyo  ikiwa ni kilomita 8 tu ilipo mradi wa viwanja wa Kilomo.

"Mradi huu wa Kilomo ambao Mimi kama balozi wa vijana RealEstate.ni sehemu ambayo itakuwa Kwa Kasi kiuchumi kutokana na kuwepo karibu na bandari ya kisasa Bagamoyo ambayo hivi karibuni unenzi wake unaanza hivyo ni vyema wananchi wakaichangamkia fursa hii Kwa kumiliki viwanja kwa bei nafuu" alisisitiza Kitenge.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Vijana Real estate, Azaidu Daudi amesema kampuni hiyo imedhamiria kumwezesha kila mtanzania apate fursa ya kumiliki kiwanja kwa bei rafiki.

"Kampuni yetu ina miaka mitatu tangu ianzishwe na tumekuwa tukiuza viwanja maeneo tofauti nchini ikiwemo Bunju, Mbezi Mpigi Majohe, Madale na Mbweni na kwa sasa tunavyo viwanja Kilomo na mradi huu umechukua takribani mwaka mmoja ambapo tulikuwa tunahakiki maeneo hayo kwa kuyapima na atakayenunua atakabidhiwa hati yake” Amesema Mkurugenzi Daudi.

Aidha amesema viwanja hivyo vina ukubwa tofauti kuanzia Square mita 450 hadi 1000 na bei inaanzia milioni 4 na kuendelea na pia unaweza kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha miezi 6 na ukikamilisha malipo unakabidhiwa hati yako.

Hata hivyo amesema lengo lao ni kutaka kila mmoja amiliki kiwanja hivyo watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani viwanja hivyo vipo sehemu nzuri ambayo huduma zote muhimu zinapatikana.


Comments