Kanisa la TAG ilala kuadhimisha jubilee ya miaka 50.

 

Kanisa la TAG ilala kuadhimisha jubilee ya miaka 50.



Na Mwandishi wetu, Dar es salaam.

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la TAG ilala Dkt Titius Mkama amesema February 11 Mwaka huu wanatarajia kufanya maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya tokea kuanzishwa kwa kanisa hilo mwaka 1973.

Akizungumza ofisini kwake Jijini Dar es salaam Dkt mkama amesema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kumshukuru Mungu kwa kazi kubwa ya Umishioni walioifanya kwa kuwahubiria kweli ya neno lake, watu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali Dunia atika kipindi chote tokea kuanzishwa kwake.

Pia amesema kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali ya kusaidia  jamii ikiwemo,kuchangia damu,semina kwa vijana,kutembelea watoto yatima.

"Tunawakatibisha watu wote kuja kuungana nasi siku hiyo,karibuni sana, hakuna kiingilio ni mtu mwenyewe na miguu yake au nauli yake basi. Kwahiyo tunawakaribisha sana" Alisema Dkt Makama.

Dkt Titius amebainisha kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Askofu mkuu wa Makanisa ya Assembles of God Tanzania (TAG) Dkt Barnabas Mtokambali,kadhalika kutakuwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali Ambayo kuna matawi ya Kanisa la TAG ikiwemo Congo DRC,Rwanda na Malawi.

Jubilee hiyo ya miaka 50 itafanyika katika viwanja vya shule ya msingi

Comments