KEMMON SPORTS AGENCY KUWAKUTANISHA ULINGONI TONNY RASHID NA BONDIA 'MSOUTH' USIKU WA VITASA DAR, KIDUNDA NAYE NDANI

 

KEMMON SPORTS AGENCY KUWAKUTANISHA ULINGONI TONNY RASHID NA BONDIA 'MSOUTH' USIKU WA VITASA DAR, KIDUNDA NAYE NDANI. 






Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

Kampuni ya Kemmon sports Agency inayojushughulisha na michezo ya aina mbalimbali hapa nchini inatarajia kumkutanisha ulingoni bondia ambaye anatajwa kuwa namba Moja Kwa sasa hapa nchini Tonny Rashid dhidi ya bondia kutoka nchini Afrika ya kusini Sabelo Ngebinyana kutetea mkanda wake wa ubingwa wa Afrika.

Mkurugenzi wa Kemmon Sports Agency ambaye pia ni promota wa pambano hilo Sada Salum amewaambia waandishi wa habari  kuwa pambano hilo litapigwa katika ukumbi wa Ubungo plaza Jijini Dar es salaam February 24,2023 ambapo pia litaambatana na mapambano mengine makubwa mawili ikiwemo kupambania mkanda wa kitaifa wa TPBRC

Amesema kuwa pambano lingine ni kati ya mkali wa ngumi Selemani Kidunda kuzichapa na Patrick Mukala  (DRC) wakiwania mkanda wa ABU uzito wa Super Middle

Aidha promota huyo ameyataja mapambano mengine ya utangulizi yatakayopigwa usiku huo kuwa ni pamoja na pambano la Emmanuelle Mwakyembe atakayepigana na Fransis Miyeyusho, Mbaraka Mtange dhidi ya Hamza Mchanjo, Mwinyi Msangela dhidi ya Ajemi Amani, Hemed Pelengela dhidi ya Iddy Pazzi huku mwanadada Halima bandola akizuchapa dhidi ya mwanadada Florah Malechela 

Hata hivyo promota huyo amewataka wakaazi wa jiji la Dar es salaam na mashabiki wa mchezo huo,kununua tiketi zao katika vituo mbalimbali ikiwemo Vunjabei store na Vunjabei total ili Kushuhudia pambano hilo huku akiwatoa wasiwasi wale watakaoshindwa kuhudhuria pambano hilo kukaa majumbani mwao na kuliangalia kupitia Azam TV ambao watalirusha Mubashara(Live).

Mabondia hao pia wamepima uzito na afya zao hii leo katika hoteli ya Kebby iliyopo Bamaga ambao ni Moja ya wadhamini wa pambano hilo. 

Mapambano hayo ya ngumi "vitasa night" yatapigwa katika ukumbi wa Ubungo plaza Jijini Dar es salaam, February 24,2023 kuanzia saa 12 jioni. 







Comments