KIDUNDA KAMKACHA BONDIA MKONGOMANI?PROMOTA WA PAMBANO AFUNGUKA MAZITO,AKASIRISHWA NA HATUA YA BONDIA HUYO KUTOTOKEA "FACE OFF"

  KIDUNDA KAMKACHA BONDIA MKONGOMANI?PROMOTA WA PAMBANO AFUNGUKA MAZITO,AKASIRISHWA NA HATUA YA BONDIA HUYO KUTOTOKEA "FACE OFF"






NA MWANDISHI WETU.

Amemkacha mpinzani wake?ndivyo ambavyo unaweza kusema mara baada ya bondia Mjwtz Selemani Kidunda kushindwa kutokea kwenye kwenye uwanja wa Las Vegas,Mabibo wakati wa zoezi la "FaceOff" ambapo mabondia wote wawili hupima uzito na kutambiana mbele ya umati wa mashabiki zao.

Hatua hiyo imeleta sintofahamu kwa Mpinzani wake Raia wa (DRC)Patric Mukala baada ya kutojitokeza katika zoezi la kupima uzito  kwenye maandalizi ya Pambano la ngumi za kulipwa linalotarajiwa kufanyika Kesho Februari 24 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam wakiwania mkanda wa ABU uzito wa super middle.


Akizungumza mara baada ya kupima uzito Mabondia wengine Mkurugenzi wa Kampuni Kemmon Agency ambaye pia ni  Promota wa Pambano hilo Sada Salim amesema  amesikitishwa sana na kitendo alichofanya Selemani Kidunda kwani walishasainiana Mkataba hivyo Pambano lipo palepale na asipotokea atatakiwa kulipa fedha alizopewa na fidia kutokana na kukiuka Mkataba wa makubaliano yao.


Sitofahamu hii imekuja baada mpinzani wa Kidunda kupanda jukwaani na kupima uzito lakini baada ya mshereheshaji wa zoezi hilo kumwita zaidi ya mara 3 Kidunda si yeye wala wapambe wake Waliojitokeza uwanjani hapo hali iliyomlazumu kwa muda Mpinzani huyo kutofanya (Face off) mpaka Mpinzani wake awepo na mpaka raia huyo wa DRC anaondoka uwanjani  hakutokea


"Selemani Kidunda acha Woga njoo uwanjani uonyeshe Umwamba wako Ulingoni usiogope kupigwa hata Tyson alivuma sana kushinda kila Pambano lakini aliwahi kupigwa acha janja janja tunataka tuone vitasa "amesema Promota Sada 

Aidha promota huyo amewataka mashabiki wa mchezo huo kuendelea kununua tiketi zao katika maeneo yaliyotangazwa ambapo pambano hilo la kukata na shoka pia litarushwa live na kituo cha luninga cha Azam tv kuanzia saa 1 jioni.

 Katibu wa kaminsheni wa ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC)Yahya Poli amesema  mpaka leo hawana taarifa yeyote ya udhuru kutoka kwa  Selemani Kidunda na wameshangazwa na hatua ya kutotokea katika zoezi hilo hivyo kulingana na sheria ya ngumi za kulipwa shirikisho hilo litachukua hatua dhidi yake.

Aidha ameongeza kuwa kama mpaka kufikia saa 8 mchana wa leo kama bondia Seleman Kidunda hatotokea shirikisho litachukua maamuzi magumu.

Comments