SAU YAZINDUA KAULI MBIU YAKE 'SALA NA KAZI' KUELEKEA 2025,YASEMA HOFU YA MUNGU NI MUHIMU KWA TAIFA.

 SAU YAZINDUA KAULI MBIU YAKE 'SALA NA KAZI' KUELEKEA 2025,YASEMA HOFU YA MUNGU NI MUHIMU KWA TAIFA. 

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha sauti ya umma (SAU)Bertha Mpata akizungumza wakati alipokuwa akizindua kauli mbiu ya chama hicho ambayo wataenda nayo mpaka mwaka 2025.

Karibu mkuu wa chama cha sauti ya umma (SAU)Makalio Kyara akizungumza wakati wa uzinduzi wa kauli mbiu ya chama hicho jijini Dar es salaam

Viongozi mbalimbali wa chama cha sauti ya umma,SAU wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kauli mbiu hiyo.


Na Thadei PrayGod, Dar es salaam. 


Chama Cha Sauti ya umma, (SAU) kimezindua kauli mbiu yake "Sala na Kazi" ambayo kitaitumia mpaka mwaka 2025.


Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa kauli mbiu hiyo Jijini Dar es salaam  mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Bertha Mpata amesema kuwa kauli mbiu ya "Sala na Kazi" imekuja baada ya chama kufanya utafiti na kujidhihirisha kuwa sasa ni wakati Kwa watanzania kuwa na hofu ya Mungu mioyoni mwao.


Amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu Kwa kutambua kwamba Mungu ndiye msingi wa kila jambo, hatua ambayo itachochea maendeleo.


Aidha mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kauli mbiu hiyo itakuwa ni Moja ya sera za chama hicho kuelekea 2025.


Kwa upande wake katibu mkuu wa chama Cha SAU, Majalio Kyara amesema kuwa kupitia kauli mbiu ya 'sala na kazi' ndipo watanzania watapata uponyaji hasa ukizingatia nyakati za sasa ambazo maadili yameporomoka Kwa kiasi kikubwa. 


Akizungumzia hatua ya Rais kuruhusu mikutano ya kisiasa, Bw Kyara amesema ni hatua nzuri na yenye maslahi mapana Kwa siasa za Tanzania hivyo chama hicho pia kinatarajia Kuanza mikutano yake hivi karibuni ikiwa ni baada ya mfungo wa Kwaresma Kwa waumini wa dini ya Kikristo pamoja na Mwezi mtukufu wa Ramadhan Kwa waimini wa dini ya kiislam kumalizika. 


Aidha katika hatua nyingine chama Cha Sauti ya umma (SAU)kupitia Kwa katibu mkuu huyo kimeishauri serikali ya Tanzania kuungana na watanzania katika kutoa pole kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililozikumba nchi za Syria na Uturuki Kwa kutengeneza mfumo ambao utamwezesha walau kila mtanzania kuchangia hata shilingi elfu Moja ili kutoa pole Kwa nchi hizo kufuatia janga hilo.


Kuhusu suala la mfumuko wa bei Bw Kyara ameishauri serikali kutumia jitihada kubwa na za haraka katika kutatua mfumuko huo wa bei Kwa bidhaa mbalimbali za chakula ikiwa ni pomoja na kuhakikisha wakulima wa Tanzania wanalima mazao ya kutosha ya chakula.

Comments