SILENT WITNESS' MOVIE INAYOMZUNGUMZIA TAJIRI ALIYEENDA JELA ILI KUMNUSURU BINTIYE AMBAYE ALIMUUA MAMA YAKE WA KAMBO.

 SILENT WITNESS' MOVIE INAYOMZUNGUMZIA TAJIRI ALIYEENDA JELA ILI KUMNUSURU BINTIYE AMBAYE ALIMUUA MAMA YAKE WA KAMBO. 






Lin Mengmeng (Deng Jiajia), binti wa mfanyabiashara maarufu, tajiri na mwenye majivuno Lin Tai (Sun Honglei), anatuhumiwa kumuua mama yake wa kambo, mwimbaji maarufu aitwaye Yang Dan, baada ya kugundua kuwa mama yake huyo wa kambo alikuwa akimsaliti baba yake mara Kwa mara ,  kwenye video ya tukio hilo anaonekana Binti huyo akibishana na mamake wa Kambo na baadaye kuingia ndani ya gari yake na Kisha kumgonga na kusababisha mauti ya Mama huyo.

Babake Binti ambaye ni tajiri Bwana,  Lin Tai anadai binti yake hana hatia anaajiri wakili anayelipwa pesa nyingi zaidi nchini China aitwaye , Zhou Li (Yu Nan) ambaye hakuna kesi aliyowahi kushindwa maishani wakili ambaye anaweza kuugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo,

 huku mashtaka ya umma yakisimamiwa na Tong Tao (Aaron Kwok), wakili mahiri na rekodi isiyo na doa, ambaye amekuwa hakuwahi kumpenda mfanyabiashara huyo Lin Tai kwa miaka mingi hatimaye anasimamia kesi hiyo upande wa  mashtaka ambayo hayajathibitishwa bado  Lakini baada ya video za CCTV na ushuhuda mkuu uliotangulia, kuonyesha ni kweli Binti huyo alimuua Mama yake wa kambo Kwa Kumgonga na gari katika siku ya kwanza ya kesi iliyotangazwa sana, na hata Binti kukiri Mbele ya waendesha mashtaka kuwa yeye ndiye aliyemuua mamake wa Kambo wakili aliyekodiwa na babake kumtetea anaigeuza kesi hiyo kufikia hitimisho rahisi sana kwamba dereva wa baba yake Kwa zaidi ya Miaka 15  ndiye mkosaji(muuaji)na hata baada ya derega huyo.naye kuishangaza mahakama Kwa kusema yeye ndiye aliyemuua Mama wa kambo wa Binti huyo , ukweli unaanza kufichuka huku upande wa utetezi na mwendesha mashtaka ukiweka makucha ya ukweli. na upokee vidokezo kutoka kwa chanzo kisichoeleweka kuhusu kile kilicho chini ya mwonekano wa wazi.

Ukweli ambao wakili adui wa Baba yake anauweka wazi kuwa Baba huyo ndiye aliyemuua mkewe na Kisha kumtengenezea kesi bintiye na mahakama ikaamini ushahidi huo na Kisha kumuunganisha mfanyabiashara huyo kwenye kesi ya mauaji ya mkewe na Kisha kumwachilia huru Binti yake.

Lakini baadaye wakili wake anagundua kuwa ni kweli binti wa mfanyabiashara huyo alimuua Mama yake wa kambo lakini baba yake Kwa upendo aliyonao kwa bintiye alitengeneza mashahidi wa uongo Ili kumtetea Binti yake asiende jela na baada ya janja hiyo kustukiwa na wakili asiyempenda mfanyabiashara huyo ndipo baba huyo alipotengeneza video nyingine fake ambapo alimtafuta msichana aliyefanana na binti yake na mwingine akifanana na mkewe ambaye ni marehemu na kulitengeneza eneo fake la parking kama ile ya kwenye video ya kwanza ikimuonyesha Binti akimgonga mama yake ambayo ilionyeshwa mahakamani. 

Lakini Kwa wakati huu video hiyo fake Inamwonyesha Binti yake huyo kuwa ni kweli alimgonga mama yake wa kambo na gari lakini hakufa na kwenye video hiyo anaonekana tajiri huyo akimfuata mama huyo pale alipodondokea na kumpigiza kichwa kwenye chuma ukutani kisha mama huyo kufariki Dunia hivyo mahakama inamkuta na hatia tajiri huyo ambaye anakweda jela licha ya yeye kutomuua mkewe lakini anafanya hayo yote ili kumuokoa Binti yake ambaye ni kweli alimuua mamake wa kambo asiende jela. 

Comments