VIDEO YA "UMEYAKANYAGA" YAMUINGIZA MANDONGA KWENYE SINGELI, KUZINDULIWA USIKU WA LEO DAR.

 

VIDEO YA "UMEYAKANYAGA" YAMUINGIZA MANDONGA KWENYE SINGELI, KUZINDULIWA USIKU WA LEO DAR. 

3
Bondia Karim MANDONGA, wa kwanza kulia, akiwa na msanii wa singeli chubby Love aliyekaa katikati sambamba na meneja wa msanii huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa umeme bei pia, G maker wakizungumza na waandishi wa habari juu ya video mpya ya msanii huyo inayozinduliwa leo Dar es salaam

NA MWANDISHI WETU

Ni kama vile bondia maarufu Kwa sasa hapa nchini Karim Mandonga ameingia rasmi kwenye muziki hasa wa singeli baada ya bondia huyo kuonekana Kwa mara ya kwanza kwenye video ya Singeli ya msanii wa Muziki huo Chudy Love ambaye leo Februari 17, 2023 anatarajia kuzindua video ya wimbo wake mpya unaojulikana kama “Umeyakanyaka”, ambao humo ndani bondia Karim Mandi ga 'mtu kazi' ameonekana akizipiga na msanii huyo 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Chudy Love amesema kuwa video ya wimbo huo ambayo tayari imeshatoka kwenye platform mbalimbali za muziki itazinduliwa rasmi hii leo katika show yake matata ambapo pia atauimba wimbo huo mbele ya mashabiki zake itakayofanyika Small Planet (Sinza) kuanzia majira ya saa 2 usiku.

Hata hivyo Chubby Love ametoa shukrani zake Kwa bondia Karim Mandonga kwa kuunga mkono muziki wake kwamba ameona kipaji kikubwa  kwake ndiyo maana amemsapoti katika harakati zake.

“Namshukuru Mandonga kwa kunisapoti katika muziki wangu, kipo kitu amekiona kwangu na kunitangaza, twendeni YouTube tukauone wimbo huo na niwakaribishe baadaye hapa Small Planet,” amesema Chudy Love.

Kwa upande wake Mandonga amempongeza Mkurugenzi wa Umeme Bei Poa G Maker kwa kumsapoti msanii huyo.

Amesema kwamba ametoa sapoti kubwa kwenye shoo ya Chudy Love ambayo itaambatana na utambulisho wa video mpya ya wimbo wa “Umeyakanyaga”.

“Anayemdiss huyu msanii kwa wimbo wake wa Umeyakanyaga hatuangalii, sisi tunachosema ni wakati wa Mungu ndio sahihi,” amesema Mandonga.

Naye Mkurugenzi wa Umeme Bei Poa ambaye pia ni Meneja wa Msanii huyo G Maker ameeleza kufurahishwa na uwepo wa Mandonga katika utambulisho wa wimbo huo.

“Mandoga ameingia kwenye muziki kwenye wimbo unaojulikana kama Umeyakanyaga, na leo kutakuwa na usiku wa Umeyakanyaga,” amesema G Maker.

Comments