MANDONGA,NYUMBA FASTA YAWAPA DILI WAPANGAJI DAR.

 MANDONGA,NYUMBA FASTA YAWAPA DILI WAPANGAJI DAR.



NA MWANDISHI WETU.

Bondia maarufu hapa nchini Karim Mandonga 'mtu kazi' Amewataka watanzania kuzitumia kampuni ambazo hazina janja janja katika kupangisha au kununua nyumba katika maeneo mbalimbali nchini


Mandonga ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika mkutano baina ya  kampuni ya Nyumbafasta ambayo inajihusisha uuzaji na upangishaji wa nyumba,mashamba na viwanja bila kutumia dalali.

Aidha Mandonga amesema kuwa kupitia kampuni hiyo sasa Watanzania wataweza kupata nyumba za kupanga bila kutoa fedha za mwezi mmoja kama makato ya dalali.

Kampuni haina madalali, ukitaka nyumba unapata kwa kodi inayohitajika, ukitaka nyumba usihangaike na matapeli na ili kuepuka matapeli tumia Nyumbafasta, hutalipa kodi ya mwezi mmoja kwa dalali,” amesema Mandonga na kuongeza,



Kwa upande wake Afisa Masoko wa Nyumbafasta Robinson Marley amebainisha kwamba Nyumbafasta ni mfumo wa kidijitali unaokuwezesha kupata nyumba za kupanga bila malipo ya kodi ya  mwezi mmoja na kupata mawasiliano ya mwenye nyumba mojakwamoja kwa gharama ndogo kuanzia shilingi elfu moja.

Vilevila amesema Nyumbafasta inakuwezesha kununua au kuuza nyumba au ardhi zilizohakikiwa wauzaji ili kujiepusha na migogoro. 

“Nyumbafasta imetengenezwa na vijana wa kitanzania na inapatikana mtandaoni Tanzania nzima kupitia tovuti ya  www.nyumbafasta.co.tz kwa kutumia simu janja(smartphone) mwenyenyumba anaweza kusajili nyumba yake na mpangaji anaweza kutafuta nyumba ya kupanga kokote pale Tanzania,” ameongeza Marley.

Naye Meneja w Uendeshaji wa Nyumbafasta Alex Chambika amesema kupitia Nyumbafasta mpangaji anaweza kupata nyumba yenye ubora kwa gharama nafuu, kwamba Mfumo huu ni rahisi kuutumia kwa kuwa umetengenezwa na vijana waandisi wazawa wanaojua Watanzania wanahitaji nini.

“Mfumo huu unasaidia kuokoa muda ambao mpangaji anautumia kupata nyumba vilevile mfumo huu unasaidia kuepusha migogoro isiyo ya lazima wakati wa kununua nyumba au ardhi,” ameeleza Chambika.

Kwamba Nyumbafasta inakitengo cha huduma kwa wateja kinachotoa huduma bora na kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kwa wakati.

Hivy9 ametoa wito kwa wenyenyumba za kupanga Tanzania nzima kujisajili kupitia tovuti yetu www.nyumbafasta.co.tz na kupitia mawakala wetu wa nyumbafasta watakao kuwa wakifanya kampeni ya usajii ya mtaa kwa mtaa kwanzia mkoa wa Dar es Salaam.

“Tunawakaribisha kutumia nyumba fasta kwenye huduma ya ununuzi na upangaji wa nyumba bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja,”amesema.

Comments