Skip to main content

MBIO ZA HISANI ZA PUGU MARATHON KUFANYIKA MAY 27 MWAKA HUU,JIMBO KUU KATOLIKI DAR LASEMA ITAKUWA HISTORIA

MBIO ZA HISANI ZA PUGU MARATHON KUFANYIKA MAY 27 MWAKA HUU,JIMBO KUU KATOLIKI DAR




NA PRAYGOD THADEI.


 Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thadaeus Ruwa’ichi, O.F.M amesema kuwa jimbo hilo limeandaa Mbio za hisani zijulikanazo kama Pugu MARATHON

Askofu Ruwa'ichi ameyasema hayo alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari mapema hivi leo jijini Dar es salaam juu ya ujio wa Mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya kwanza.

Askofu huyo  amesema lengo la kuu la mbio hizi ni kusaidia kupata majitoleo kwa ajili ya kuendeleza kituo chao cha hija kinachopatikana Pugu, kudumisha afya pamoja na kujenga utamaduni wa michezo.

Aidha ameongeza kuwa mbio hizo zitakuwa zikifanyika wiki ya mwisho ya mwezi May kila mwaka huku akiangazia umuhimu wa mbio hizo ambazo pia zinaangalia eneo la Pugu kama eneo la kihistoria la kanisa hilo tangu kuja kwa wamishionari wa kwanza waliofika eneo hilo na baadaye kuanzishwa kwa shule ya kidato cha 5 na 6 ya Pugu na hata harakati za kupata uhuru zilizoanzishwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia akifundisha na kuishi katika shule hiyo.

Hata hivyo ameongeza kuwa lengo la Mbio hizo ni kukusanya kiasi cha shilingi milioni 400 ambazo zitatumika katika kuboresha kituo cha hija kilichopo Pugu,pamoja na kusaidia katika hospitali 

Mbio hizo zitakuwa za aina nne ambazo ni matembezi ya kilomita 2 ada ya ushiriki shilingi 20,000, mbio fupi za kilomita 5 ada ya ushiriki 20,000, mbio za kilomita 10 ada ya ushiriki 30,000, na mbio za kilomita 21, ada ya ushiriki 30,000.

Aidha amewaomba wadau wa michezo  kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizi. Pia mashirika, makampuni, wafanyabiashara na washikadau wengine kujitokeza kutufadhili ili tuweze kufanikisha lengo kuu la mbilo hizi,” ameongeza Askofu Mkuu Ruwa’ichi

Comments