MUFTI WA TANZANIA AIOMBA SERIKALI KUONDOA KODI KWENYE TENDE,KATIKA MFUNGO WA RAMADHAN
MUFTI WA TANZANIA AIOMBA SERIKALI KUONDOA KODI KWENYE TENDE,KATIKA MFUNGO WA RAMADHAN
NA MWANDISHI WETU.
Mufti Sheik Zubeir ameyasema hayo katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhan lililofanyika katika viwanja vya Karimjee lililoandaliwa na baraza kuu la waislamu (Bakwata)Mkoa wa Dar es Salaam
Alisema kuwa katika kipindi cha mfungo wa Ramadhan mwaka jana waislamu nchini walipata tabu kupata bidhaa za tende katika maeneo mbalimbali kutokana na bidhaa hiyo kutopatikana kwa urahisi kwa kuuzwa kwa bei ghali hivyo kama serikali itaondoa kodi kwa bidhaa hiyo itasaidia upatikanaji wake
Kuhusu mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii,Mufti amewataka maimamu wa misikiti kote nchini kurejesha madarasa maalum katika misikiti yao ambayo yatatoa elimu ya dini kwa watoto na vijana ili kurejesha maadili ya kitanzania ambayo yameonekana kuporomoka kwa siku za hivi karibuni.
Alisema ili kujenga maadili yaliyo bora waislamu nchini wanatakiwa kuzingatia yale yote walioagizwa na mola wao kupitia Quran tukufu,sambamba na kufanya yote yaliyo mema.
Kwa upande wake Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye ofisi yake ndiyo iliyoandaa kongamano hilo la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan alisema ofisi yake itahakikisha kila wilaya inakuwa na msikiti wa wilaya sambamba na kubainisha mpango wake wa kuongeza misikiti kila mtaa ili waumini wa dini ya kiislam kuendelea kuwa karibu na mola wao.
Sheikh Walid aliongeza kuwa katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani waislamu wanatakiwa kujenga utamaduni wa kusaidiana na kuwasaidia pia wale wasiojiweza utamaduni ambao akiwasisitiza kuuendeleza hata baada ya kumalizika kwa mfungo huo.
Kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan Mkoa wa Dar es salaam pia lilihudhuriwa na Masheikh Mbalimbali ambao pia walitoa mawaidha na kuwasisitiza waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kumcha mola wao akiwemo Sheikh Kipoozeo,Sheikh Mziwanda,Sheikh Issa Othman pomoja na viongozi wengine wa dini ambao pia wote kwa pamoja walisisitiza upendo
Comments