Skip to main content

MZEE MPILI ALAMBA SHAVU,DAR QUALITY MOTORS.

 MZEE MPILI ALAMBA SHAVU,DAR QUALITY MOTORS.








KAMPUNI inayojihusisha na uuzaji wa vifaa vya magari Dar Quality Motors leo imemtangaza mzee Mpili kama balozi wa kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,Afisa masoko wa kampuni hiyo BI Shemsa Said Msellem amesema kuwa waliamua kumpa mzee huyo maarufu hapa nchini kwani wanaamini ana ushawishi mkubwa katika jamii na ataitangaza vyema kampuni hiyo.

Bi Msellem amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ni miongoni mwa makampuni mahiri ya uuzaji wa vifaa na vipuri vya magari hapa Tanzania hivyo kwa sasa wanaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Naye balozi wa kampuni hiyo Mzee MPILI ameishukuru kampuni hiyo kwa kumchagua kama balozi ambapo ameongeza kuwa ataitumia vyema nafasi yake katika kuitangaza kampuni ya Dar Quality Motors.

Aidha amewakaribisha watanzania kutumia kampuni hiyo kuagiza vifaa vya magari vilivyo bora.

Comments