PUMA ENERGIES TANZANIA YAWAZAWADIA MAFUTA, MITUNGI YA GESI WANAWAKE WENYE ULEMAVU WAKISHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
PUMA ENERGIES YAWAZAWADIA MAFUTA, MITUNGI YA GESI WANAWAKE WENYE ULEMAVU WAKISHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah akimkabidhi mtungi wa gesi dereva bajaji Sophia Abdallah jijini Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma imeungana na Watanzania wote nchini katika kusheherekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kila Machi 8 ya kila mwaka kwa kutoa zawadi ya Mafuta, pamoja na mitungi ya gesi ya kilo sita kwa wanawake wenye ulemavu ambao wanajihusisha na utoaji huduma ya kusafirisha wananchi kwa kutumia usafiri wa bajaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 8, 2023 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah amesema wamefanya hivyo kwa kutambua nafasi ya wanawake hao wenye ulemavu wanaofanya shughuli hizo katika jiji la Dar es Salaam.
Hivyo amesema Kampuni ya Puma imeona kuna kila sababu ya kuungana na wanawake hao kuadhimisha siku hiyo lengo likiwa ni kutambua mchango wao sambamba na kuwapa moyo kwamba Ulemavu walionao sio sababu ya kuwa wanyonge.
“Kampuni ya Mafuta ya Puma tunajihusisha na biashara ya Mafuta, vilainishi, pamoja na nishati safi ya gesi ya kupikia. Siku ya leo tumeamua kutoa zawadi ya kuwajazia Mafuta wanawake wenye Ulemavu ambao wanatoa huduma ya kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam. Lakini mbali na kujaza Mafuta full tank tunawapa na zawadi ya mtungi wa gesi kila mmoja. Tunataka wanapofanya shughuli zao wasifikirie watapika kwa jiko gani,” amesema Fatma na kuongeza,
“Lakini kutoa zawadi ya mitungi ya gesi kwa wanawake hawa wenye ulemavu ni kitumia siku hii kuungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha nishati safi ya kupikia na kuachana na kuni na mkaa, hivyo pamoja na mambo mengine tunatumia siku hii ya wanawake duniani kihamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia,”.
Kwa upande wake Sophia Abdallah dereva bajaji mmoja wa wanufaika wa zawadi hizo, ameishukuru Puma kwa kiwajazia mafuta full tank na kuwapagia mitungi ya gesi ya kipikia.
Amewahamasisha akina mama nchini kwa kuwataka kuwa wapambanaji na kutumia gesi ya Puma.
- Get link
- X
- Other Apps



Comments