TANZANIA ANNUJUUM ISLAMIC CENTER KUFANYA MASHINDANO MAKUBWA YA QURAN DAR JUMAPILI HII,WAZIRI ULEGA MGENI RASMI.

 TANZANIA ANNUJUUM ISLAMIC CENTER KUFANYA MASHINDANO MAKUBWA YA QURAN DAR JUMAPILI HII,WAZIRI ULEGA MGENI RASMI.




NA MWANDISHI WETU

KITUO ChanTanzania Annujuum Islamic Centre kwa kushirikiana na Al Madrasati Nnujuum wameandaa Mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu Kitaifa ya Madrasa yatakayoshirikisha Madrasa Bingwa za Mikoa Mbalimbali Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mlezi wa Madrasati Nnujuum ambaye pia ni mtangazaji wa vipindi vya michezo vya redio E FM,Maulid Kitenge amesema kuwa mashindano hayo ya kuhifadhi Quran tukufu yanatarajiwa kufanyika jumapili ya March 26,2023 katika ukumbi wa DYCC YEMEN ulipo Chang'ombe jijini Dar es salaam. 

Aidha amesema kuwa kwenye fainali za Mashindano ya kuhifadhi Qur'an Takatifu yanayofanyika kitaifa Kwa kukutanisha madrasa zote nchi nzima mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega.

KITENGE amesema Kituo Cha Tanzania Annujuum Islamic Centre ambayo imeandaa Mashindano hayo ikiwa lengo ni kuwafanya watoto waweze kuhifadhi Qur'an Takatifu kote nchini ambapo pia atahudhuriwa na mimi watu mashuhuri pia.

Aidha amesema kuwa kuhifadhi Qur'an Takatifu Kwa watoto wadogo inasaidia Kwa kiasi kikubwa kujifunza tabia njema na maadili mazuri ya kidini wakiwa katika umri mdogo.

"Tunatarajia Mgeni rasmi atakua Abdallah Ulega Waziri wa Mifugo na uvuvi kwani amewahi kujifunza madrasa akiwa mdogo,hivyo zitakuwa fainali za aina yake kwasabubu pia kutakuwepo na wageni mbalimbali mashuhuri," amesema Kitenge.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Madrasati Nnijuum Mustafa Ally amebainisha kwamba lengo la kuzikutanisha madrasa zote nchini kwenye shindano hilo ni kubadilisha muonekano wa tafsiri za madrasa kuwa zinafundisha mambo yasiyofaa Kwa watoto,nakuifanya jamii itambue kuwa madrasa zinafundisha maadili mazuri Kwa watoto.

"Ndugu zangu waandishi wa habari fainali hizo zimegawanyika katika makundi manne ambapo kundi la kwanza nila watoto wanaohifadhi juzuu 3, kundi la pili Juzuu 15,kundi la tatu Juzuu 20 na Kundi la nne Juzuu 30 " amesema Naibu  Katibu Mkuu huyo wa Madrasati.

Nakuongeza kwamba" Washindi wa Kila kundi watapata zawadi ambapo hatutazitaja hapa itakua ni surprise siku hiyo hivyo naomba watu Wajitokeze Kwa wingi kushuhudia Mashindano hayo ambayo yanafanyika Kwa mara ya kwanza Kwa kushindanisha madrasa zote nchi nzima na tunatarajia yatakuwa endelevu.

Nae Irene Kilenga maarufu kama Baby Mama ambaye pia ni Mlezi wa Madrasati Nnijuum amesema kuwa katika kipindi hiki Cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Mashindano hayo yatasaidia kutekeleza Ibada ya Funga Kwa Waumini wa Kiislam, hivyo amewaomba wazazi na walezi wajitokeze kushuhudia namna watoto wao wanavyoshindana kuhifadhi Qur'an Takatifu.

Comments