TCRA YAZITAKA TAASISI KUDHIBITI TAKA HATARISHI.

 

TCRA YAZITAKA TAASISI KUDHIBITI TAKA HATARISHI.

******************
Timothy Marko 

SERIKALI imewataka wadau wa sekta ya mawasiliano kuzitunza nakuzitekeza taka hatarishi zinazotokana na vifaa vya kieletroniki.

Akizungumza katika kongamano la wadau wa sekta ya Mawasiliano pamoja na watendaji wa wizara ya Habari Teknolojia na Mawasiliano jijini Dar es salaam Waziri wa wizara hiyo Nape Moses Nauye amesema kuwa Takwimu zataka hatarishi zinazotokana na Mabaki ya vifaa vya masiliano zimekuwa zikiongezeka hali inayo pelekea hatari za kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

" Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya taka milioni7.7 za kieletroniki huzalishwa mwaka hadi mwaka".Alisema Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia Nape Nauye.

Waziri Nape alisema kuwa lengo la kongamano hilo zinazojumuisha nchi 17 zakutoka Afrika nikuona nijinsi gani za kuzipunguza taka hizo kwa kutunga sheria na miongozo ya punguza taka hizo.

Alisema lengo nikuona Matakwa ya kisheria yanafuatwa katika kuteketeza taka hizo.

"Nchi za Afrika Mashariki zimekuja Tanzania ikiwa Tanzania ni mwenyeji kujadili namna yakutokomeza na kuziharibu taka za kieletroniki ".Aliongeza waziri Nape Moses Nauye. 

Mkurugenzi mkuuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk Jabir bakeri amesema kuwa kwa kushirikiana nataasisi ya umoja Mawasiliano Tanzania ECO Dk Ally Simba amesema kuwa taasi hiyo kwa kushirikiana na nchi 7wanajadili namna yakudhiti taka hizo.

Alisema Taka hizo zimekuwazikiambatana na madini hatari kwa walaji na watumiaji. 

"Taka hizi ni hatarishi kwa sababu zimeambata na madini hatarishi '".Alisema Dk Ally Simba.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawassiliano Tanzania (TCRA) Dk Jabir Bakari amezitaka taasisi mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu kuzifanyia tafiti taka hizo hatarishi ilikuweza kuondokana natatizo lauharibifu wa mazingira.

Comments