TUICO YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WAANDAMIZI WA TAASISI ZA KAZI NCHINI,SERIKALI YAWAUNGA MKONO
TUICO YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WAANDAMIZI WA TAASISI ZA KAZI NCHINI, SERIKALI YAWAUNGA MKONO
![]() |
Naibu waziri,ofisi ya waziri mkuu,Vijana,ajira na wenye elemavu Patrobasi Katambi akizungumza wakati alipokuwa akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa TUICO na ATE kwa viongozi waandamizi wa taasisi za kazi iliyofanyika katika hoteli ya New African Jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara,taasisi za fedha ,huduma na Ushauri (TUICO) Paul Sangeze akizungumza katika washa hiyo. |
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi amesema kuwa wizara hiyo kupitia ofisi ya waziri mkuu ipo tayari kusimamia na kutekeleza sheria za Wafanyakazi zilizowekwa na kama kuna taasisi ya serikali haitekelezi sheria hizo itafuatiliwa.
Aidha amesema Serikali itaendelea kuheshimu mikataba ya Kimataifa kwa kuhakikisha kuwa inaweka ulinzi na Usalama mahali pa kazi ili kusaidia Wafanyakazi walioajiriwa au kujiajiri wanafanya kazi zao kwa amani kwa maslahi mapana ya Ustawi wa Jamii na uchumi wa taifa .
Hata hivyo amesema serikali ina imani na sekta binafsi kwani ndio wanaochangia zaidi katika sekta ya ajira nchini hivyo kutoa mchango mkubwa katika Uchumi wa nchi na kipato cha mtu mmoja mmoja .
“Warsha hii ya leo haijawahi kutokea ni kwa mara ya kwanza naamini hiyo chachu na kiungo muhimu cha ushirikiano wa Waajiri, Wafanyakazi pamoja na taasisi za kifedha katika kutekeleza maazimio ya Shirika la kazi Duniani ILO ili kuboresha mazingira rafiki katika eneo la kazi”Amesema Waziri Katambi.
Sambamba na hayo amewaasa huu viongozi wa vyama hivyo kutoingiza siasa ka lakinitika vyama vyao kwani Wana uwezo wa kukaa pamoja na kusuluhisha palipo na shida baina yao na serikali siyo kama miaka ya nyuma ambapo ilikuwa vigumu kufanya majadiliano hivyo kwa sasa wanapokea maoni yao na kutatua changamoto zao bila kuhusisha wanasiasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wa Viwanda biashara,taasisi za fedha ,huduma na Ushauri (TUICO) Paul Sangeze amesema Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi waandamizi waliohudhuria katika warsha hiyo watasaidia kuongeza uelewa katika taasisi zao.
Aidha amesema warsha hiyo itakuwachachu katika usimamizi wa sheria na haki za Wafanyakazi ikiwemo kufanya majadiliano kabla ya maamuzi ambayo yanaweza kuiletea hasara taasisi na kuboresha mazingira mahala pa kazi.
Naye Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Naomba amesema Waajiri wana haki ya kujiunga na Chama cha Wafanyakazi kwani ipo kikatiba mtu binafsi hashurutishwi anajiunga kwa hiari yake mwenyewe na anatakiwa afuate utaratibu.
Hata hivyo amesema Waajiri ni Wadau wakubwa hivyo ushirikiano huo utasaidia kutatua changamoto mahala pa kazi na ni vyema mikataba yote ya kazi ifanyike kwa uwazi na majadiliano yafanyike kwa nia njema pande zote mbili ziridhike.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara,taasisi za fedha ,huduma na Ushauri (TUICO) Paul Sangeze akizungumza katika washa hiyo.

Comments