WAKAZI WA DAR 'KU-ENJOY TAMASHA LA PASAKA BILA MALIPO VIWANJA VYA LEADERS APRIL 9,2023
WAKAZI WA DAR 'KU-ENJOY TAMASHA LA PASAKA BILA MALIPO VIWANJA VYA LEADERS APRIL 9,2023
Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama Akizungumza na waandishi pembeni Mratibu wa Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa
Na mwandishi wetu
Maandalizi ya Tamasha la pasaka yamepamba moto kuelekea kilele cha Tamasha hilo tarehe 09 April 2023 katika viwanja vya leaders club kinondoni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Msama Promotion kinondoni Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema "Maandalizi ya Tamasha hilo yanakwenda vizuri na waimbaji mbalimbali wanaoshiriki kwenye tamasha hilo wameendelea kutambulisha na leo tunatambulisha Christopher Mwahangila"
Msanii wa muziki wa injili Christopher Mwahangila(Kushoto) akiongea mbele ya waandishi pembeni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na wa mwisho (kulia) ni Mratibu wa Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa.
Pia Msama amesema kuwa Tamasha litakuwa la aina yake litakalowajumuisha watu wa dini na madhehebu yote na kwamba watu wote wanakaribishwa kwenye tamasha hilo.
"kila Mtanzania anakaribishwa kuongeza jitihada zinazofanywa na mama kwa kuwa alipokea nchi akiwa kwenye kipindi kigumu lakini bado tunafuraha, Upendo na amani katika Taifa letu hivyo tamasha hili sio la kukosa njooni tumpongeze mama kwa pamoja" alisema Alex Msama
Kwa upande wake mwimbaji wa nyimbo za injili Christopher Mwahangila ameahidi kutoa Burudani Safi na kukonga nyoyo za Watanzania hususani wapenzi wa nyimbo za injili ambapo amechukua fursa hiyo kuwakaribisha watu wote katika tamasha hilo.
"Tamasha la pasaka litakonga nyoyo za waumini mbalimbali wa nyimbo za injili na nitaimba live usipange kukosa, lakini pia tujitokeze katika kumpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya miaka miwili, njooni tusifu kwa pamoja" amesema Christopher Mwahangaila
Naye Mratibu wa Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa amesema kuwa Maandalizi yote ya Tamasha hilo yamekamilika huku akiwaomba watu wote kuwahi kwenye tamasha hilo ambapo vyakula na vinywaji inapatikana viwanjani hapo kwa Bei nafuu.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments