Skip to main content

WANAOTAKIWA KUHAMA BONDE LA MSIMBAZI KUPISHA MRADI WA UBORESHAJI WAKE WAHAKIKISHIWA FIDIA, UHAKIKI KUMALIZIKA IJUMAA IJAYO

 

WANAOTAKIWA KUHAMA BONDE LA MSIMBAZI KUPISHA MRADI WA UBORESHAJI WAKE WAHAKIKISHIWA FIDIA, UHAKIKI KUMALIZIKA IJUMAA IJAYO



Mratibu wa Miradi ya DMDP pamoja na Mradi wa Kuendeleza Bonde la Mto Msimbazi Mhandisi Humphrey Kanyeye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

WAKAZI wanaotakiwa kuhama katika Bonde la Mto Msimbazi wametakiwa kuwa watulivu kwamba kila mtu anayestahili atalipwa fidia yake.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Miradi ya DMDP pamoja na Mradi wa Kuendeleza Bonde la Mto Msimbazi Mhandisi Humphrey Kanyenye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi baada ya kuibuka kwa baadhi ya wakazi hao kulalamika kwamba fidia ni ndogo.

Mhandisi Kanyeye amesema kwamba Serikali haipo tayari kumdhulumu mtu yeyote haki yake, hivyo kama kuna mtu mwenye malalamiko anatakiwa kuyaripoti kwenye dawati la malalamiko ili yafanyiwe kazi.

“Kama kuna malalamiko yapelekwe kwenye dawati la malalamiko na utasikilizwa, na kama hutaridhika nenda mahakamani, lakini kulalamika kiholela ni kuleta taharuki,” amesema Mhandisi Kanyeye.

Hivyo ameeleza kwamba kwa sasa wanaendelea na uhakiki wa thamani zinazoathirika na mradi huo ili kujua gharama ya fidia ambayo kila mtua anastahili kulipwa.

Kwamba katika zoezi hilo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wamashafanyiwa uthamini wa mali zao na wamekubaliana na fidia walizowekewa na wapo wachache waliolataa, lakini wanaendelea kushughulikia jambo hilo.

“Kimsingi walitakiwa wasilipwe kwani walishapewa notisi tangu mwaka 1979 kwasababu eneo hilo ni hatarishi, lakini Serikali kwa kujali imeamua walipwe, hata hivyo hatuwezi kulipa kitu ambacho hakipo,” amebainsha Mhandisi Kanyenye.

Mhandisi Kanyeye amesema kwamba wanalipa thamani ya mali iliyopo kwa sasa na sio vinginevyo na kueleza kuwa wao baadhi ya wananchi wenye matarajio makubwa kuliko uhalisia.

Comments